State House Blog

Mkutano Mkuu wa UVCCM Dodoma Chuo cha Mipango.

 • MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,alipowasili katika Ukumbi wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Dodoma Chuo cha Mipango.
 • MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Taifa John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM,katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma, akitowa nasaha zake kwa Wagombea na Wajumbe wa mkutano huo

Mkutano Mkuu wa Tisa wa UWT Kikwete Hall mjini Dodoma

 • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasili katika ukumbi wa mkutano wa Mkuu wa UWT Kikwete Hall mjini Dodoma akiongozana na Katibu Mkuu wa UWT Amina Makilagi na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Salama Aboud Talib
 • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa katika meza kuu akiwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakishangiria wakati akitangazwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa UWT katika ukumbi wa Kikwete Hall

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema katika sherehe ya upokeaji msaada kwa kikundi cha SIRI MOYO

 • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akitoa hotuba mara baada ya kukabidhi msdaada wa Vyarahani kwa Ushirika wa akina Mama (SIRI MOYONI) Unguja Ukuu Kae pwani Wilaya ya Kati Unguja.kulia yake ni Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico na kushoto yake ni Mke wa Balozi mdogo wa China aliopo Zanzibar Mama Liu Jie.
 • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kushoto akiwa pamoja na Mke wa Balozi mdogo wa China aliopo Zanzibar Mama Liu Jie wakikabidhi msaada wa Vyarahani kwa Ushirika wa akina Mama (SIRI MOYONI) Unguja Ukuu Kae pwani Wilaya ya Kati Unguja.
 • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa katika picha ya pamoja na viongozo na Wnaushirika akina Mama (SIRI MOYONI) Unguja Ukuu Kae pwani Wilaya ya Kati Unguja.

Dk.Shein amewaapisha Wakuu wa Mikoa wapya pamoja na Naibu Katibu Mkuu

 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein,akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib Hassan,hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman Abdallah , hafla hiyo imefanyika Ikulu
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Mwanajuma Majid Abdallah
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali baada ya kumalizika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Mikoa na Naibyu Katibu Mkuu Ikulu

Dk.Shein Ahudhuria Mazishi ya Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikali Zanzibar Othman Bakari

 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na wakijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar katika Sala ya Kuuombea Mwili wa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikali Zanzibar Marehemu Othman Bakari,dua ikisomwa na Sheikh Fadhil Soraga katika Masjid Shurba kidingochekundu Zanzibar na kuzikwa katika makaburi ya mwanakwerekwe
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi la mareheme Othman Bakari, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikali Zanzibar, maziko hayo yamefanyika katika makaburi ya mwanakwerekwe Zanzibar.