State House Blog

Dk.Shein amewaapisha viongozi mbali mbali alio wateua hivi karibuni

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.George Joseph Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla alikuwa Mrajis wa Mahkama Kuu ya Zanzibar
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Kubingwa Mashaka Simba kuwa Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bibi Aziza Iddi Suwedi kuwa Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,
  • Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Khamis Juma Maalim,
  • Baadhi ya Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar ni miongoni mwa Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya kiapo cha Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar walioapishwa leo na Viongozi wengine kazi iliyofanya na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,
  • Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar wakipitia hati zao za viapo kabla ya kuapishwa Rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kushika wadhifa walioteuliwa hafla ya kiapo ilifanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Khamis Ramadhan Abdala kuwa Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar