State House Blog

Ufunguzi wa barabara ya Jendele-Cheju- Unguja Ukuu

 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la Uzinduzi wa Baraza ya Jendele hadi Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja, kulia Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe na kushoto Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib, hafla hiyo imefanyika katika barabara hiyo jendele ikiwa ni shamrashamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 54.
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikata Utepe kuashiria uizindu wa barabara mpya kutoka jendele hadi Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja, hafla hiyo imefanyika katika eneo la jendele Wilaya ya Kusini Unguja.
 • KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe akisoma taarifa ya kitaalamu ya Ujenzi wa Mradi wa Barabara ya Jendele hadi Unguja Ukuu wakati wa ufunguzi wa barabara hiyo ikiwa ni shamrashamra za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa hafla ya uzinduzi wa barabara mpya ya kiwango cha lami kutoka Jendele hadi Unguja Ukuu, ikiwa ni shamrashamra za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • WANANCHI wa Kijiji cha Jendelea wakishangilia wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo wakiwa na Watoto wao wakishiriki katika hafla hiyo.
 • MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Hassan Khatib akitowa neno la shukrani wakati wa hafla ya uzinduzi wa barabara ya Jendele hadi Unguyja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja. ikiwa ni shamra shamra za sherehe za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • WANANCHI na wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa barabara ya Jendele hadi Unguja Ukuu, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akihutubia katika viwanja vya cheju Mkoa wa Kusini Unguja.
 • BAADHI ya Wageni waalikwa katika hafla ya Uzinduzi wa Barabara ya Jendele hadi Unguja Ukuu wakifuatilia hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya cheju Mkoa wa Kusini Unguja.
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Balozi Ali Karume wakati wa hafla ya uzinduzi wa barabara ya Jendele hadi Unguja Ukuu.
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembea baada ya kuizindua barabara ya Jendele hadi Unguja Ukuu iliojengwa kwa kiwango cha lami, ikiwa ni shamra shamra za sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • BAADHI ya Wageni waalikwa katika hafla ya Uzinduzi wa Barabara ya Jendele hadi Unguja Ukuu wakifuatilia hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya cheju Mkoa wa Kusini Unguja.
 • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Balozi Ali Karume, alipowasili katika kijiji cha jendele kwa ajili ya Uzinduzi wa Barabara ikiwa ni shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanziba.