Media » News and Events

Dk.Ali Mohamed Shein ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kwa mafanikio iliyoyapata.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.

Alimpongeza Balozi Seif kwa kuiongoza vyema Ofisi hiyo licha ya kuwa ni na kuwa na mambo mengi na Idara nyingi lakini ameweza kuiongoza vyema na kuweza kupata manufaa kutokana na kuwa ndio Ofisi inayoratibu masuala ya Serikali.Dk. Shein alieleza matarajio yake kuwa juhudi zaidi zitaendelea kuchukuliwa na uongozi wa Ofisi hiyo ili Serikali iendelee kupata tija na mafanikio bora zaidi huku akitumia fursa hiyo kueleza jinsi Zanzibar ilivyopiga hatua katika kuimarisha mapato yake hatua iliyopelekea kufanya mambo yake mengi wenyewe..

Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi huo kwa kuwasilisha vizuri MpangoKazi wake na kusisitiza kuwa kikao hicho kinatoa fursa nzuri katika kutekeleza vyema majukumu ya kazi zao pamoja na kutatua matatizo mbali mbali.Aidha, Dk. Shein alisisitiza haja ya kufanya kazi kwa kujituma ili Ofisi hiyo iendelee kuleta sifa na kuendelea kumsaidia Makamo wa Pili wa Rais katika kutekeleza majukumu yake .

Nae Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd aliipongeza uongozi wa Ofisi hiyo kwa kukusanya taarifa nzuri na kuwasilisha katika kikao hicho kwa ufaisi ulio bora huku akiitaka Ofisi hiyo ijiandae vyema katika kikao kijacho kama hicho sambamba na kuwapongeza viongozi na watendaji wa Ofisi hiyo.

Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alimpongeza Rais Dk. Shein kwa namna anavyoiongoza Zanzibar ambapo kila mmoja anashuhudia mageuzi makubwa ya utendaji wa kazi kwa watumishi hasa katika sekta ya umma.Aliongeza kuwa mageuzi hayo yamechochea kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi katika sekta zote ambapo wasaidizi wake wote wanazingatia sana miongozo na maelekezo yake katika kutekeleza majukumu yao ya kusimamia shughuli za Srrikali katika maeneo yao.

Nao uongozi wa Ofisi hiyo ulieleza kufarajika kwao na hatua za Dk. Shein za kuanzisha na kuendeleza vikao hivyo ambavyo vimekuwa vikiwasaidia sana viongozi na watendaji wa ofisi hiyo katika utekelezaji wa kazi zao pamoja na mafanikio yaliofikiwa na Serikali katika kutoa huduma mbai mbali katika jamii zikiwemo huduma za watu wenye ulemavu.

Nae Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee aliupongeza uongozi wa Ofisi hiyo kwa uwasilishaji mzuri wa Mpangokazi wake na kusisitiza haja ya uongozi huo kujitahidi ili kuonesha taswira nzuri ya Makamu wa Pili wa Rais pamoja na Ofisi yenyewe.