Media » News and Events

Dk.Shein ametuma pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Uganda,

Salamu hizo zilieleza kuwa wananchi wa Zanzibar wanaungana na ndugu zao wa Jamhuri ya Watu wa Uganda katika kusherehekea siku hii adhimu kwa Taifa hilo.

Aidha, katika salamu hizo, Dk. Shein alimuhakikishia Rais Museveni kuwa Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano mkubwa uliopo kati yake na Jamhuri ya Watu wa Uganda sambamba na kuimarisha udugu uliopo kati ya wananchi wa Jamhuri ya Watu wa Uganda na wananchi wa Zanzibar.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alisisitiza juu ya haja ya kufanya kazi kwa pamoja katika kuimarisha mashirikiano katika masuala mbali mbali yanayohusu Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika pamoja na masuala mbali mbali ya kimataifa.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alitumia nafasi hiyo kumtakia uongozi mwema Rais Museveni pamoja na kumtakia uonghozi mwema wa Taifa hilo kwa amani na utulivu kwa maendeleo endelevu ya wananchi wa Jamhuri ya
Watu wa Uganda.