News and Events

Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kurudi nchini leo akitoa nchini Indonesia


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kurudi nchini leo akitoa nchini Indonesia ambapo alihudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (I0RA), akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.

Mheshimiwa  Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kurudi nchini leo akitoa nchini Indonesia

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Soekarno- Hatta, mjini Jakarta Indonesia, Dk. Shein aliangwa na Viongozi mbali mbali wa nchi hiyo.
Dk. Shein alihudhuria Mkutano huo wa siku tatu ulioanza tarehe 05 Machi na kufikia kilele chake Machi 07 mwaka huu, mjini Jakarta Indonesia ambao ulitanguliwa na vikao vya Mawaziri na wadau wengine kutoka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ya nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA).
Katika Mkutano huo, Dk. Shein alifuatana na viongozi mbali mbali akiwemo Mama Mwanamwema Shein, pamoja na viongozi wengine wa Serikali ya Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania na Seikali ya Mapainduzi ya Zanzibar.