News and Events

Rais wa Zanzibar na MBLM Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-


Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua NDUGU ALI SAID BAKARI kuwa NAIBU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA KUDHIBITI UTAFUTAJI NA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA ZANZIBAR. Kabla ya uteuzi huo Ndugu Ali Said Bakari alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Idara ya Nishati, Zanzibar.

Uteuzi huo unaanzia tarehe 20 Aprili, 2017.