News and Events

Mheshimiwa Dk.Ali Mohamed Shein amefanya Uteuzi


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Omar Zubeir Ismail kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mamlaka ya Kudhibiti Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo Bwana Omar Zubeir alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Idara ya Nishati, Zanzibar. Uteuzi huo umeanza leo tarehe 18 Machi 2017