News and Events

U T E U Z I


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:

U T E U Z I

1. MWENYEKITI WA BARAZA LA CHUO CHA UTAWALA WA UMMA
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 5(1)(a) cha Sheria ya Chuo cha Utawala wa Umma Namba 1 ya mwaka 2007, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bibi Fatma Said Ali kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Cha Utawala wa Umma.

2. MWENYEKITI WA BODI YA KAMISHENI YA WAKFU NA MALI YA AMANA.
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Namba 2 ya mwaka 2007, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Prof. Hamad Rashid Hemed Hikmany kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana.

3. MWENYEKITI WA BODI YA UWAKALA WA ULINZI WA JKU
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Uwakala wa Ulinzi ya JKU Namba 2 ya mwaka 2015, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Kanal Mstaafu Makame Mbarouk Hassan kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uwakala wa Ulinzi wa JKU.

Uteuzi huo umeanzia tarehe 2 Septemba, 2017.