Publications

HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MBLM DK, SHEIN KATIKA UZINDUZI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI,


HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHESHIMIWA DK. ALI MOHAMED SHEIN KATIKA UZINDUZI WA BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI,
TAREHE 5 APRILI, 2016

Mheshimiwa Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar,

Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Zanzibar,

Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi,

Waheshimiwa Mabalozi Wadogo mliopo, Zanzibar,

Wawakilishi wa Mashirika mbali mbali ya Kimataifa mliopo,

Waheshimiwa Viongozi wa Vyama vya Siasa,

Ndugu Wageni Waalikwa,

Mabibi na Mabwana,

Assalamu Aleikum,

UTANGULIZI:

Naanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu; Mtukufu, Muumba wa Ulimwengu na vyote vilivyomo, kwa kuturuzuku neema ya uhai, afya na uwezo wa kukutana leo hii tarehe 5 Aprili, 2016, katika tukio hili muhimu kwa mustakbali wa nchi yetu na maendeleo ya wananchi wake. Tunawaombea dua wenzetu waliotangulia mbele ya haki,  Mwenyezi Mungu awasamehe makosa yao na awape malazi mema peponi.  Kadhalika, kwa wale wenzetu waliopata mtihani wa maradhi mbali mbali, tunamuomba Mola wetu awape uzima, ili waendelee kushirikiana nasi katika shughuli za ujenzi wa Taifa letu.

Attachment: attachment hotuba_ya_brazala_wawakilishi