Publications

Hotuba ya Rais Dk.Ali Mohamed Shein,katika maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar


HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, MHE. DK. ALI MOHAMED SHEIN, KATIKA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, AMAAN STADIUM TAREHE 12 JANUARI, 2016

Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan;
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa;
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad;
Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar,

Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi;
Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar,

Mheshimiwa Mzee Ali Hassan Mwinyi;
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mheshimiwa Benjamin William Mkapa,
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete;
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mheshimiwa Dk. Salmin Amour Juma;
Rais Mstaafu wa Zanzibar,

Mheshimiwa Dk. Amani Abeid Karume;
Rais Mstaafu wa Zanzibar,

Waheshimiwa Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,

Mheshimiwa Job Ndugai;
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho;
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar,

Mheshimiwa Othman Chande Mohamed;
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mheshimiwa Omar Othman Makungu;
Jaji Mkuu wa Zanzibar,

Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa,

Mheshimiwa Abdalla Mwinyi Khamis;
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,

Viongozi mbali mbali wa Serikali na Vyama vya Siasa,

Ndugu Wananchi,

Mabibi na Mabwana,

Assalamu Aleikum,

Awali ya yote, napenda nianze kwa kumshukuru Mola wetu Mtukufu mwenye kustahiki kushukuriwa na viumbe vyote kwa kutujaalia uhai na afya njema tukaweza kukutana katika hadhara hii muhimu kwa historia na harakati za maendeleo ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano waTanzania kwa jumla.  Leo tarehe 12 Januari, 2016 tunaadhimisha kilele cha sherehe za miaka 52 tangu yalipofanyika na kufanikiwa kwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964.

Attachment: attachment sherehe