Publications

Hotuba ya Mhe. Rais kwenye Baraza la Eid el Fitri


HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, MHE. AL HAJJ DK. ALI MOHAMED SHEIN,KATIKA BARAZA LA IDD EL FITRI JULAI, 2016 (1 SHAWWAL, 1437)
BISMILLAHI RAHMANI RAHIM

Shukurani zote anastahiki Mola wetu Mtukufu Subhana Wataala; Muumba wa Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo ndani yake. Tunakiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi kuwa Yeye peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa kwa haki. Na kwake Yeye ndiyo marejeo yetu sote. Tumuombe Mwenyezi Mungu atupe khatma njema katika marejeo yetu.Sala na salamu zimshukie Mtume wetu Muhammad (S.A.W), Aali zake, Sahaba zake na waumini wote waliofuata njia yake ya uongofu. Inshaallah na sisi tuwe miongoni mwao. Tunamuomba Mola wetu (SW) atuwezeshe kuyatekeleza maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake ili tuweze kufanikiwa hapa duniani na huko akhera twendako.

Attachment: attachment HOTUBA_IDD_EL_FITR