Dk.Hussein Mwinyi ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Uhamiaji la Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ikiwa ni Shamrashamra za Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mshauri Elekezi kutoka Wakala wa Majengo Zanzibar Mhandisi Hassan Haji Mrisho, akitowa maelezo ya Kitaalamu ya ujenzi wa Jengo la Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, linalojenwa katika eneo la Mazizini Unguja, ikiwa ni Shamrashamra za Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.