Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo ameungana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan na Viongozi mbali mbali wa Kitainfa katika Ibada ya kuuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Elias John Kwandikwa aliyekua Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.Tukio lilifanyika katika viwanja vya Karimjee,Jijini Dar es Salaam.

Dkt.Mwinyi amemzungumzia Marehemu Kwandikwa kama kiongozi aliyekuwa wa Mfano na kielelezo cha Uongozi bora huku akisema Taifa limegubikwa na Majonzi makubwa.

Akizungumzia Marehemu,Rais Dkt.Mwinyi alisema katika uhai wake marehemu Kwandikwa alikuwa Waziri wa kwanza kumtembelea Ikulu Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha na kwa hakika walifanya kazi kwa karibu sana.

Dkt.Mwinyi akimuelezea alimuelezea Marehemu kwa umahiri wake kwa kusema ...