State House Blog

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akizungumza na Wajasiriamali Wanawake katika wiki ya Maadhimisho ya UWT Wilaya ya Mjini Unguja.

 • MKE wa Rais wa Zanzibar na MBLM Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa UWT alipowasili katika viwanja vya Kituo cha Amali Miembeni kuhudhuria Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).
 • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimsikiliza Mjasiriamali wa Kikundi cha Kibibi Product.Bi.Priscilla Tayari akitowa maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na Kikundi hicho, wakati akitembelea maonesho ya Wajasiriamali Wanawake wa Wilaya ya Mjini Unguja katika Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) yaliofanyika katika viwanja vya Kituo cha Amali Miembeni Zanzibar na (kulia kwake) Makamu Mwenyekiti wa UWT.Mhe.Thuwaiba Editon Kisasi.
 • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwaangaliwa Wanafunzi wa darasa la upambaji wa Chuo cha Amali Miembeni wakiwa katika maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) yaliofanyika katika viwanja vya chuo hicho cha UWT Wilaya ya Mjini Unguja na (kulia) Mkuu wa Chuo Ndg. Said Kheri Ame na Makamu Mwenyekiti wa UWT Mhe Thuwaiba Editon Kisasi
 • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimsikiliza Mjasiriamali wa Kikundi cha Chuo cha Wajasiriamali Wilaya ya Mjini kinachojishughulisha na utengenezaji wa losheni Bi.Rauhiya Abdalla Khamis, wakati akitembelea maonesho ya Wajasiriamali Wanawake wa Wilaya ya Mjini Unguja katika Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) yaliofanyika katika viwanja vya Kituo cha Amali Miembeni na (kulia kwake) Makamu Mwenyekiti wa UWT Mhe Thuwaiba Editon Kisasi.
 • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimsikiliza Mjasiriamali wa Kikundi cha Kibibi Product.Bi.Priscilla Tayari akitowa maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na Kikundi hicho, wakati akitembelea maonesho ya Wajasiriamali Wanawake wa Wilaya ya Mjini Unguja katika Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) yaliofanyika katika viwanja vya Kituo cha Amali Miembeni Zanzibar na (kulia kwake) Makamu Mwenyekiti wa UWT.Mhe.Thuwaiba Editon Kisasi.
 • MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chuo cha Amali UWT Zanzibar ambae pia ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Mgeni Hassan Juma, akizungumza wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania.(UWT) yaliofanyika katika viwanja vya Chuo cha Amali Miembeni Mjini Unguja
 • BAADHI ya Wabunge na Wawakilishi kupitia nafasi za UWT Wilaya ya Mjini Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wajasiriamali Wanawake wa Wilaya ya Mjini Unguja, wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Wiki ya UWT yaliofanyika katika viwanja vya Chuo cha Amali cha UWT Miembeni Unguja.
 • MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mhe.Thuwaiba Editon Kisasi akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya UWT yaliofanyika katika viwanja vya Chuo cha Amali Miembeni Zanzibar,kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Mke wa Rais wa Zazibar Mama Mariam Mwinyi,kuzungumza na Wajasiriamali Wanawake.
 • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi Cheti Muhitimu wa Chuo cha Amali cha UWT Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja Bi.Sumaiya Ali Shaib,baada ya kumaliza Mafunzo ya Upishi katika chuo hicho,ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya UWT, yaliofanyika katika viwanja vya Chuo hicho.
 • WANACHAMA wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakimshangilia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) wakati akihutubia katika Maadhimisho ya Wiki ya UWT, yaliofanyika katika viwanja vya Chuo cha Amali Miembeni Zanzibar.
 • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi Cheti Mwanafunzi wa Chuo cha Amali cha UWT Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja Ndg. Soud Haji Juma, baada ya maliza mafunzo yake ua Ushoni katika Chuo hicho, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya UWT, yaliofanyika katika viwanja vya chuo hicho.
 • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwahutubia Wajasiriamali Wanawake wa vikundi mbali mbali na Wanachama wa UWT Wilaya ya Mjini Unguja katika hafla ya Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) yaliofanyika Miembeni Zanzibar.