State House Blog

RAIS WA ZANZIBAR ALHAJ DK.HUSSEIN MWINYI AMEONGOZA WANANCHI WA ZANZIBAR KATIKA KISOMO NA DUA YA KUMUOMBEA MAREMEMU SHEIKH ABEID AMANI KARUME LEO.

  • SHEIKH.Jaffar Abdalla Ramadhan akihitimisha kisoma cha Hitma na dua, ya kumuombea Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh. Abeid Amani Karume, iliyofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 7-4-2023.
  • MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akisoma dua baada ya kumalizika kwa kisomo cha hitma na dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh. Abeid Amani Karume,iliyofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja leo 7-4-2023 na (kulia kwa Mufti) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango na Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhaj.Dkt. Amani Karume na (kushoto kwa Mufti Mkuu ) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.
  • BAADHI ya Wananchi waliohudhuria kisoma na dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh.Abeid Amani Karume, wakiitia dua ikisoma na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (hayupo pichani) kisomo hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar
  • MAMU Mkuu wa Msikiti wa kwa Mtoro Dar es Salaam Sheikh. Abass Ramadhan akitowa mawaidha wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh.Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, baada ya kumalizika kwa dua na kisomo cha hitma cha kumuombea marehemu kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja leo 7-4-2-23
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika katika kuitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha hitma na dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh.Abeid Amani Karume iliyofanyika leo 7-4-2023,katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar na ((kulia kwa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhaj Dkt. Amani Karume na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa