State House Blog

Rais wa Zanzibar Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Wananchi katika Maziko ya Marehemu Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk,Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume.(hayupo pichani)baada ya kumalizika kwa maziko ya Marehemu Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar. Haji Omar Haji na (kulia kwa Rais) Jaji Mkuu wa Zanzibar Alhaj. Omar Othman Makungu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Wadi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, wakijumuika katika kuitikia dua ya kumuombea marehemu.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa Sala ya kuuswalia mwili wa Marehemu Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar Haji Omar Haji, iliofanyika katika Masjid Noor Kombeni Wiliya ya Magharibi ‘B’ Unguja.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi katika maziko ya Marehemu Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar Haji Omar Haji, yaliofanyika katika Kijiji cha Shakani Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja.
  • WANANCHI wakihudhuria maziko ya Marehemu Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar Haji Omar Haji yaliofanyika katika makaburi ya Kijiji cha Shakani Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana wa Jaji Mkuu wa Zanzibar Alhaj Omar Othman Makungu baada ya kumalizika kwa maziko ya Marehemi Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar. Haji Omar Haji, yaliofanyika katika makaburi ya Shakani Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja