State House Blog

Rais wa Zanzibar Mhe.,Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Viongozi wa Dini Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Ikulu.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Sheikh Hassan Othman Ngwali kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 12-5-2022.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisaini hati ya kiapo ya Sheikh Hassan Othman Ngwali, baada ya kumuapisha kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
  • SHEIKH Hassan Othman Ngwali akiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
  • MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwake) Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar.Mhe Mahmoud Mohammed Mussa,Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar na Viongozi wa Dini walioteuliwa hivi karibu kushika nafasi ya Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali na Sheikh.Othman Ame Chum, wakiwa katika ukumbi wa Ikulu wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa wa Zanzibar na Tanzania na wa Afrika Mashariki kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
  • SHEIKH Hassan Othman Ngwali akisoma hati ya kiapo kabla ya kuapishwa kushika nafasi ya Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) na (kushoto kwake) Sheikh. Othman Ame Chum aliyeteuliwa kuwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 12-5-2022.Jijini Zanzibar
  • MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akizungunza na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, wakiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa kwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Naibu Kadhi Mkuu iliyofanyika leo 12-5-2022.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar wakati wa kupigwa kwa wimbo wa Taifa wa Zanzibar, Tanzania na Wimbo wa Afrika Mashariki kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa kwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 12-5-2022.