State House Blog

Ziara ya kutembelea Visima vya Maji safi na Salama Bumbwisudi Wilaya ya Magharibi “A” Unguja.

  • Rais wa Zanzibar na MBL Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kulia) akizungumza na Wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya Visima vya Maji Safi na Salama (ZAWA) Bumbwisudi Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi wakati alipofanya ziara ya ghafla.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo kwa watendaji wakati alipofanya ziara ya Ghafla kwa kutembelea visima vya Maji Safi na Salama Bumbwisudi Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa Mjini Magharibi (katikati) Waziri wa Maji,Nishati na Madini Mhe.Suleiman Masoud Makame,(wa tatu kulia) Mkuu wa Wilaya ya Magharibi"A" Mhe.Suzan Peter Kunambi.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji,Nishati na Madini Mhe. Suleiman Masoud Makame pamoja na watendaji wengine wakati alipofanya ziara ya Ghafla kwa kutembelea visima vya Maji Safi na Salama Bumbwisudi Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa Mjini Magharibi.
  • Mlinzi katika Visima vya Maji Safi na Salama (ZAWA) Bw.Hussein Ismail akitoa changamoto zinazowakabili katika kazi zao wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipofika maeneo ya Visima vya Maji Safi na salama (ZAWA)Bumbwisudi Wilaya ya Magharibi"A" Mkoa wa Mjini Magharibi kuangalia tatizo lililopelekea kukosekana kwa huduma hiyo.