Hafla hiyo iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud,Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Mwinyihaji Makame,Wengine ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Abubakar Khamis, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib pamoja na viongozi wengine.Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 94(4) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemteua Jaji Abdulhakim Ameir Issa kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar, uteuzi ambao umenza leo 03 Disemba, 2012 hadi 14 Januari 2013.
Wakati huo huo, Dk. Shein alikutana na Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman aliefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha.
Katika mazungumzo hayo , Dk. Shein alimuehidi Brigedia Jenerali Othman kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kutoa suhirikiano mkubwa kwake na kumpongeza kwa kuteuliwa kwake katika nafasi hiyo.Dk. Shein alimueleza Brigedia Jenerali huyo kuwa kila aina ya ushsirikiano atapewa pamoja na kuendelea kumuunga mkono katika kazi zake ili aweze kufanya vizuri kwani lengo kubwa ni kuitumikia nchi pamoja na wananchi wake.
Nae Brigedia Jenerali Othman alimuhakikishia Dk. Shein kuwa atafanya kazi zake kwa juhudi kubwa na kusema kuwa mashirikiano atakayoyapata yataweza kumsaidia zaidi katika utendaji wake wa kazi hapa nchini.Ameshikilia nafasi ya Kamanda wa Brigedi ya Nyuki (101 KV), ambaye kabla ya hapo nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Meja Jenerali Abdi Farah Mohamed ambaye kwa sasa amekuwa Mkuu wa Operesheni na Mafunzo, Makao Makuu ya Jeshi la Wananachi Tanzania.