Dk. Shein alisema kuwa hatua hiyo inatokana na azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kukuza mashirikiano na uhusiano na Vietnam hasa kwa kuanzisha ziara za kimafunzo kwa viongozi na wataalamu wa pande zote mbili hasa ikizingatiwa kuwa tayari Vietnam ina uzoefu mkubwa juu ya sekta hiyo.Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa wataalamu wote wa pande mbili hizo watakaa pamoja kwa lengo la kuandaa programu maalum zitakazosaidia sekta hiyo ya ufugaji ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu vijana ili waweze kupanua soko la ajira kwa kujiajiri wenyewe hasa kwa vile Zanzibar ni visiwa vilivyozungukwa na bahari.Aidha, Dk. Shein aliueleza uongozi wa Chuo hicho kuwa miongoni mwa mada kuu zilizozungumzwa kati yake na Rais wa nchi Mhe. Truog Tan Sang ni pamoja na kuimarisha mashirikiano katika sekta ya kilimo na uvuvi kati ya Zanzibar na Vietnam.
Nao uongozi wa chuo hicho ulieleza kuwa uko tayari na wazo hilo la Dk. Shein na kumueleza jinsi taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1963, ilivyopiga hatua katika tafiti zake mbali mbali juu ya ufugai wa samaki.Akitoa maelezo kwa Rais pamoja na wajumbe wengine waliohudhuria hafla hiyo fupi katika taasisi hiyo, Dk. Phan Thi Van alieleza kuwa jinsi taasisi hiyo inavyotoa elimu kuanzia ngazi za chini hadi kufikia Shahada ya Uzamifu katika fani hiyo na kuweza kupata mafanikio makubwa.