Media » News and Events

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha viongozi mbali mbali aliowateuwa Julai 10, 2021

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Nd. Mussa Haji Ali kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha viongozi mbali mbali aliowateuwa Julai 10, 2021 kushika nyadhifa tofauti katika Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Dk. Mwinyi amemuapisha Mussa Haji Ali kuwa Katibu Mkuu (OR), Ikulu pamoja na Issa Mahafoudh Haji kuwa Katibu Mkuu (OR) Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

Wengine ni Dk. Habiba Hassan Omar kuwa Katibu Mkuu (OR) Kazi, Uchumi na Uwekezaji na Mikidadi Mbarouk Mzee kuwa Naibu Katibu Mkuu (OR)  Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.

Aidha, amemuapisha Aboud Hassan Mwinyi kuwa Naibu Katibu Mkuu (OR) Fedha na Mipango anaeshughulikia Fedha na Mipango.

Miongoni mwa waliohudhuria katika hafla hiyo ni pamoja na Makamo wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Othman, Makamo wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdalla , Jaji Mkuu wa Zanzibar
Omar Othman Makungu na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmeid Said.

Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk. Mwinyi Said Haji, Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Kitwana Idrisa Mustafa, Mawaziri, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na wanafamilia