Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, akiwa na ujumbe wake, ameondoka Dar es Salaam kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Bali, I
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, akiwa na ujumbe wake, ameondoka Dar es Salaam kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Bali, Indonesia, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Indonesia na Afrika pamoja na Mkutano wa Viongozi wa Kujadili Ubia wa Maendeleo, utakaofanyika kuanzia tarehe 1 hadi 3 Septemba 2024.