Rais wa Zanzibar na Mwenyekit wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ame wahakikishia Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Afrika kuwa Zainzibar imejiandaa vema kwa Uchaguzi na utakuwa Huru wa Uwazi ,Usalama na   haki.Rais Dkt, Mwinyi ameyasema hayo alipozunguma na Waangalizi hao leo tarehe 26 Oktoba 2025 walipofika Ikulu kuonana Naye.

Rais Dkt, Mwinyi ameuambia Ujumbe huo kuwa Maandalizi ya Uchaguzi
Yamekamilika kwa mafanikio makubwa na hali ya Usalama wa Nchi ni Mkubwa na kila Mwananchi mwenye sifa atapata fursa ya kupiga kura .

Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kuwa Vyama vyote vinavyoshiriki Uchaguzi vinaendelea na mikutano ya Kampeni kwa Utulivu Mkubwa na hakuna Chama chocchote kilichowasilisha Malalamiko Tume ya Uchaguzi hali inayoonesha kukuwa kwa Demokrasia nchini.Amebainisha kuwa Nchi imekuwa na Amani na Utulivu hivi sasa kulinganisha na historia ya Chaguzi zilizopita ambapo wakati wa Uchaguzi Nchi ilikuwa na Tahadhari kubwa.

Akizungumzia Ushiriki wa Wanawake   amesema kumekuwa na Idadi kubwa ya Wanawake waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi Majimboni pamoja na Wale wa viti maalum kwa Chama Cha Mapinduzi.Makundi mengine ni Ushiriki wa Vijana ,Watu wenye mahitaji Maalum pamoja na Wagombea wa Elimu ya juu ambao Wameshirikishwa kikamilifu katika hatua zote muhimu za uchgauzi.