Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi amesema ZMBF itashirikiana na benki ya DTB Tanzania katika maeneo tofauti ikiwemo kuwasaidia wasichana kupata taulo za kike za kufua kupitia Tumaini Initiative mradi unaotekelezwa na ZMBF.
Mama Mariam Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 5 Agosti 2024 alipokutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya DTB Tanzania, Ravneet Chowdhury na ujumbe wake katika ofisi za ZMBF Ikulu Migombani.
Mama Mariam Mwinyi amewakaribisha Kampuni ya IPP Media kupitia chaneli ya televisheni ya EATV kushirikiana na ZMBF kuelimisha umma kupitia kampeni mbalimbali zinazo endeshwa na ZMBF ikiwemo ya kambi ya matibabu ya Afya Bora, Maisha Bora inayofanyika kila baada ya miezi mitatu.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi Ravneet Chowdhury ameeleza kuwa DTB itashirikiana na ZMBF kuwasaidia wasichana kupata taulo za kike ili waweze kushiriki kikamilifu katika masomo yao.