Hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi kwenye Ufunguzi wa Kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu

Hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa  Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Ufunguzi wa Kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Tarehe; 20 Oktoba, 2023

Mheshimiwa Mwenyekiti wa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu;

Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu;

Wahesimiwa Makamishna wa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu;

Waheshimiwa Wawakilishi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika,

Viongozi Mbalimbali wa Nchi na Serikali,

Waheshimiwa Mabalozi,

Wadau wa Mbalimbali wa Maendeleo,

Waheshimiwa Wenyeviti na Makamishna wa Taasisi za Kitaifa za Haki za Binadamu,

Washiriki Kutoka Taasisi Zisizo za Kiserikali

Wananchi Mliopo,

Waandishi wa Habari,

Mabibi na Mabwana,

Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutujaalia  neema ya uhai na kutuwezesha kukutana hapa leo katika hafla ya ufunguzi wa kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).Kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda nikupongeze Mheshimiwa Prof. Remy Ngoy Lumbu, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Watu kwa uongozi wako imara katika kuiongoza taasisi hii muhimu ya Umoja wa Afrika, Taasisi ambayo inalinda, inakuza na kuendeleza haki za binadamu na watu katika Bara la Afrika.

Pia, niwapongeze Makamishina wote wa Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ambao mnashirikiana pamoja katika kuimarisha haki za binadamu na watu katika bara la Afrika. HONGERENI SANA.

Ndugu Washiriki,
Kikao hiki ni matokeo ya ziara ya Mwenyekiti wa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu aliyoifanya nchini Tanzania tarehe 30 Januari, 2023, ambapo pamoja na masuala mengine yaliyojadiliwa, pia aliomba mkutano huu ufanyike hapa Tanzania. Hivyo, kwa niaba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natumia fursa hii kuwashukuru kwa uamuzi wenu wa kufanya kikao cha 77 cha Kawaida cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu hapa nchini Tanzania.

Ndugu Washiriki,
Kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote, napenda kuwakaribisha viongozi na waalikwa wote kutoka nchi mbalimbali wakiwemo; Waheshimiwa Mawaziri; Mabalozi na Viongozi wa Taasisi za Kitaifa za Haki za Binadamu na Asasi za Kiraia (AZAKI); pamoja na wawakilishi wa Serikali na makundi mbalimbali kutoka Bara la Afrika.

Nimejulishwa kuwa katika mkutano huu, yatajadiliwa masuala mbalimbali ikiwemo hali ya haki za binadamu katika bara la Afrika, taarifa za kazi za Makamishna pamoja na taarifa za mifumo ya ulinzi wa haki za binadamu Afrika. Ni matumaini yangu kuwa taarifa hizi zitatoa tathimini ya hali halisi ya haki za binadamu na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kupata mbinu za kukabiliana na changamoto zitakazoainishwa. Aidha, naamini kwamba washiriki watapata fursa ya kutoa maoni na mapendekezo yao kuhusiana na masuala yatakayojitokeza katika taarifa zitakazo wasilishwa.

Download File: