MHESHIMIWA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. HUSSEIN ALI MWINYI AMEKUTANA NA UONGOZI WA SHIRIKA LA NYUMBA TAREHE 27 FEBRURI,2023 NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WANANCHI ZILIZOWA

MHESHIMIWA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. HUSSEIN ALI MWINYI AMEKUTANA NA UONGOZI WA SHIRIKA LA NYUMBA TAREHE 27 FEBRURI,2023  NA KUSIKILIZA  CHANGAMOTO ZA WANANCHI ZILIZOWASILISHWA  KUPITIA MFUMO WA SEMA NA RAIS KUHUSU WANANCHI WALIOPANGISHWA
 
NYUMBA NA SHIRIKA LA NYUMBA

1. Ndugu Maosud Mussa Masoud ambae amemlalamikia Ndugu Abdulkarim Omar Salum kwenye nyumba Namba 10/99 iliyopo Michenzani. Mheshimiwa Rais baada kupitia vielelezo vya pande zote ametoa uamuzi wa kila mmoja apewe chumba kimoja katika nyumba hiyo.

2.Ndugu Eshe Ali Salim amemlalamikia Ndugu Abbas Abdalla Mohamed kwenye nyumba Namba 6/10 iliyopo Michenzani Mheshimiwa Rais baada ya kupitia vielelezo vya pande zote ameamua kufuatwa kwa sheria na kutokuzingatiwa matatizo yao binafsi. Kwa hivyo Nyumba No 6/10 iliyopo Michenzani amepewa Ndugu Eshe Ali Salim kwa vile ndiye aliyetambulika kwenye Mkataba wa Ukodishaji kwa sasa.

3.Feisal Ali Said amelilalamikia Shirika la Nyumba kumtoa katika nyumba Namba 239 iliyopo Hurumzi ambayo alipangishwa na Shirika hilo Mheshimiwa Rais baada kupitia vielelezo vya pande zote ametoa uamuzi wa kurejeshewa Nyumba hiyo. Ndugu Feisal Ali Said. Aidha amelitaka Shirika la Nyumba kuwatafutia nyumba nyengine wapangaji waliomo ndani ya nyumba hiyo.

4.Ndugu Imam Ali Makame amelilalamikia Shirika la Nyumba malalamiko yafuatayo kuhusiana na Nyumba Namba 781 iliyopo Hurumzi. Kuongezewa kodi kutoka Shs 250,000 mpaka shs 2,000,000 kwa mwezi kutokana na kubadilisha matumizi ya makaazi ya nyumba na kuwa ya biashara.

Kutokufidiwa gharama zake za matengenezo aliyofanya katika nyumba hiyo.

Kutokujibiwa barua yake ya maombi ya kupatiwa mkataba wa muda mrefu, Mheshimiwa Rais ametoa maamuzi na kulitaka Shirika la nyumba lifanye mawasiliano nae na wajibu barua zake kwa kufuatilia anacho kilalamikia.

5.Ndugu Gharib Ali  Issa amelalamikia  Shirika la Nyumba kwa kumtoa katika nyumba Namba 213 iliyopo Hurumzi aliyokuwa akiishi, Mheshimiwa Rais ametoa agizo kwa Shirika la Nyumba kuwasilisha barua walizomwandikia Ndugu Gharib zinazomtaka kulipa deni na akakataa kulipa deni hilo.Kutokana na kikao hicho Mheshimiwa Rais amesema hatua nyengine zitafuata.