Taarifa kwa Vyombo vya Habari 01

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya Uteuzi wa Viongozi mbali mbali katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ na Taasisi zake kama Ifuatavyo:-

1. Ndugu Silima Juma Khamis ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi.
2. Ndugu Omar Haji Gora ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Tawala za Mikoa na 
   Serikali za Mitaa.
3. Lt.Col Haji Sheha Khamis ameteuliwa kuwa Mratibu wa Idara Maalum za SMZ.
4. SP Ramadhan Khamis Ibrahim ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Viwanda vya Idara Maalum 
   za SMZ.
5. Ndugu Makame Mussa Mwadini ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa 
   Matukio ya Kijamii.
Uteuzi huo unaanzia leo tarehe 17 Septemba 2021.

Download File: