WANANCHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja waeleza kuridhishwa na juhudi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika kuwapelekea maendeleo endelevu ikiwemo miundombinu ya barabara. ameendelea kuwasisitiza wafanyabiashara kutowauzia wananchi bidhaa kwa bei ya juu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani na miezi ijayo.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Rais Dk. Shein, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Vuai Mwinyi, aliyasema hayo katika futari maalum iliyoandaliwa na Rais Dk. Shein kwa ajili ya wananchi wa Mkoa huo, futari iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Katika maelezo yake Mkuu huyo wa Mkoa alieleza kuwa wananchi wa Mkoa huo wamekuwa wakishuhudia maendeleo makuwa yanayopelekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dk. Shein.

Mkuu huyo wa Mkoa alielezaku wa miongoni mwa wananchi ambao hawatamsahau Rais Dk. Shein katika maisha yaokutokana na kuviimarishavijiji vyao kwa kuvipelekea huduma za maendeleo zikiwemo maji, umeme, skuli, barabara na vituo vya afya.

Akivitaja vijiji hivyo kikiwemo kijiji cha Mlilile, Mgonjoni, Mbuyumaji na vyenginevyo Mkuu huyo wa Mkoa alieleza kuwa wananchi wa vijiji hivyo wamefarajika kwa kupata huduma hizo muhimu za maendeleo ambazo walizikosa kwa muda mrefu.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa aliendelea kutoa shukurani hizo kwa huku akieleza jinsiwananchi wa Mkoa huo walivyo na matarajio makubwa ya kukua kwa uchumi wao kutokana na ujenzi wa barabara ya Bubu hadi Mkokotoni ambayo inaendelea na ujenzi.

Alisema kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutawasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wa Mkoa huo katika kukuza uchumi wao sambamba na kukuza uchumi wa Taifa.

Sambamba na hayo, Mkuu huo wa Mkoa huo alitoa ongezi kwa Rais Dk. Shein kwa kuendeleza utamaduni wake wa kuwafutarisha wananchi jambo ambalo alisema lina baraka na rehema kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Pamoja na hayo, Mkuu wa Mkoa huo wa Kaskazini Unguja aliwasisitiza wananchi wa Mkoa huo kuendeleza umoja na mshikamano wao ili maendeleo zaidi yazidi kupatikana.

Pia, alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa niaba ya Rais Dk. Shein kwa wananchi wote waliohudhuria katika futari hiyo aliyowaandalia na kupongeza jinsi walivyoonesha upendo mkubwa kwake wa kukubali muwaliko wake huo.

Wakati huohuo, nae Mama Mwanamwema Shein kwa upande wake aliungana na akina mama wa Mkoa huo pamoja na viongozi wanawake wa kitaifa katika futari hiyo maalum aliyoianda Rais Dk. Shein huko katika ukumbi wa Chuo hicho cha Amali Mkokotoni.

Katika hafla hiyo ya futari viongozi mbali mbali walihudhuria akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd na viongozi wengine wa dini na Serikali pamoja na wananchi mbali mbali wa Mkoa huo.

  • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dk. Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni.MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dk. Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni.