Ikulu Blog

Dk.Shein azungumza na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan,Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE) wakiwa katika ukumbi wa makadhi ya Kiongozi huyo Nchini Abu Dhabi. kulia Balozi wa Tanzania Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) Mbarouk Nossor Mbarouk.
  • Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE)akimtambulisha Mtoto Aaliyah Al Mansoori kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohahed Shein, wakati wakitoka katika ukumbi wa mkutano baada ya kumaliza mazungumzo yao.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na mwenyeji wake , Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE), baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa makadhi ya Kiongozi huyo Nchini Abu Dhabi.
  • /RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE)wakiwa katika ukumbi wa makadhi ya Kiongozi huyo Nchini Abu Dhabi.
  • VIONGOZI wa Ngazi za juu wa Serikali ya Abu Dhabi wakihudhuria hafla hiyo katika ukumbi wa makaazi wa Mfalme wakati wa mkutano huo.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE) wakitoka katika Jumba la Kiongozi huyo baada ya kumaliza mazungumzo yao.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE) baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika makaazi ya Kiongozi hiyo Nchini Abu Dhabi.

Dk.Shein Awasili Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu kwa kuaza ziara yake

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Kiongozi wa Ngazi za Juu wa nchi za Umoja wa nchi za Falme za Kiarabu( UAE) Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai kuaza ziara yake ya Wiki moja.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatana na Kiongozi wa Juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi,alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kiongozi wa ngazi za Juu wa Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai kuaza ziara yake ya Kiserikali ya Wiki moja. kushoto Balozi wa Tanzania katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu (UAE)
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Kiongozi wa Ngazi za Juu wa nchi za Umoja wa nchi za Falme za Kiarabu( UAE) Dr. Ahmad bin Abdallah Humaid Belhoul Al Falasi, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai, kuaza ziara yake ya wiki moja kulia ni Balozi wa Tanzania Katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk
  • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Mke wa Balozi wa Tanzania katika Nchi za Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Majlis Dubai

Dk.Shein ameondoka nchini kwenda nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi,kabla ya kuaza ziara yake katika Nchi za Falme za Kiarabu wakiwa katika chumba cha VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na UsaIama Zanzibar wakati wa kuondoa Zanzibar kuaza ziara yake ya Kiserikali katika Nchi za Falme za Nchi za Kiarabu.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Wazee wa CCM Zanzibar katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuaza ziara yake ya Wiki moja katika Nchi za Falma za Kiarab.
  • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuaza ziara yake ya Kiserikali katika Nchi za Falme za Kiarabu.

Dk.Shein atembelea eneo la Ujenzi wa Matenki ya Kuhifadhia Mafuta Mangapwani Zanzibar

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Ardhi Zanzibar Ahmeid Abdulrahaman Rashid, akitowa maelezo ya eneo linalotarajiwa kujengwa Matenki ya kuhifadhia Mafuta na Gesi, akionesha michoro ya eneo hilo wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya VIGOR Tofiq Salim Turky akitowa maelezo ya Ujenzi wa Kiwanda cha Gesi katika eneo la Bumbwini wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar kutembelea eneo hilo
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizunbgumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Salama Internation Refinery ,Abdallah Said Abdallah, akielezea ujenzi wa Kiwanda cha Kusafishia Mafuta Zanzibar kinachojengwa katika eneo la Mangapwani Zanzibar kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi wa ZURA Haji Kali Haji alipokuwa akimuonesha maeneo yaliotengwa kwa ajili ya ujenzi wa matenki ya Mafuta Mangapwani Wilaya ya Kaskazini B Unguja. akipata maelezo ya Mradi huo.

Taarab rasmin kusherehekea Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud alipowazili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi la zamani mnazi mmoja kuhudhuria Taarab rasmin ilioandaliwa na Kikundi cha Taifa katika ukumbi huo.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wakiwa wamesimama wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya Taarab rasmin ya kusherehekea Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni
  • KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan Kingi, akitowa maelezo kabla ya kuaza kwa Taarab rasmin ya kusherehekea Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, wakifuatilia hafla ya Taarab ya Kikundi cha Taifa cha Taraab kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
  • MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakiwa katika ukumbi wa zamani wa baraza la Wawakilishi kikwajuni wakifuatilia hafla ya Taarabu rasmin inayopingwa na Kikundi cha Taifa Zanzibar kusherehekea Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume, wakiwa katika ukumbi wa zamani wa baraza la Wawakilishi kikwajuni wakifuatilia hafla ya Taaran rasmin inayopingwa na Kikundi cha Taifa Zanzibar kusherehekea Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • MSANII wa Muziki wa Taarab Zanzibar Profesa Mohammed Elias akiimbi wimbo Wanaulizana wakati wa hafla hiyo ya kusherehekea Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi kikwajuni Zanzibar wakati Mke wa Rais wa Kwanza akitunza Mama Fatma Karume.
  • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi katika Taarab maalum ya Kikundi cha Taifa katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kusherehekea miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • MSANII Mkongwe wa muziki wa Taarab Zanzibar Makame Faki akitowa burudani wakati wa hafla hiyo akiimba Wimbo Maalum ulioombwa na wapenzi wa muziki wa Taarab Zanzibar wakati wa hafla hiyo Nampenda kwa Ishara.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mama Fatma Karume wakitunza wakati wa hafla ya Taarab rasmin ya kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
  • Baadhi ya Wananch waliohudhuria hafla ya Taarab ya kuadhimisha sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifuatilia taarab hiyo iliokuwa ikipigwa na Kikundi cha Taraab cha Taifa cha Zanzibar.
  • KIKUNDI cha Taifa cha Taarab Zanzibar kikipiga wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya kuadimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
  • BAADHI ya Mawaziri na Wananchi wakihudhuria hafla ya Taarab rasmin ya kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliofanyika katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar.
  • WACHEZAJI wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes wakiwa na Kocha wao Mkuu Hemed Suleiman Moroco wakihudhuria hafla ya Taarab rasmin ya kuadhimisha Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar.