Ikulu Blog

Rais wa Zanzibar na MBLM Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Balozi Hussein Said Khatib kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Jaji Hamid Mahmoud Hamid kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Mabrouk Jabu Makame kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bibi Rukia Mohammed Issa kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Juma Ali Juma kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Issa Mohammed Suleiman kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Ali Rajab Juma kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Joseph Abdalla Meza kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dkt,Idris Muslim Hija kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bibi Salama Mbarouk Khatibu kuwa Mkuu wa Wilaya yaMicheweni Pemba katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Kapteni Khatib Khamis Mwadini kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A.Unguja,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Abeid Juma Ali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Bakari Haji Bakari kuwa Katibu Mtendaji wa Bazara la Biashara la Zanzibar hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Ali Khamis Juma kuwa Naibu Katibu .Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Wizara ya Fedha na Mipango
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Iddi Haji Makame kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar

Rais Dkt. Shein atembelea maonesho ya Sabasaba Dar es Salaam

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko zanzibar Balozi Amina Salum Ali(wa tatu kushoto) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Map
  • Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi wa VETA kanda ya Dar es Salaam Bw. Habibu Bukko wakati alipotembelea banda la VETA
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia biashara mbali mbali za vipodozi wakati alipotembelea banda la vikundi vya Zanzibar leo katika maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali na kulia mjasiria mali Fadhil Mohamed wa Kiembesamaki Zanzibar
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia biashara mbali mbali za vipodozi wakati alipotembelea banda la vikundi vya Zanzibar leo katika maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiangalia biashara mbali mbali za viatu vya Makubadhi na Mikoba wakati alipotembelea banda la vikundi vya Zanzibar, leo katika maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipangalia mashine ya kutengenea sabuni pamoja kuapata melezo kutoka kwa Mkurugenzi George M.Buchafwe wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam leo (kulia) mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Ziwanda vidogo vidogo (SIDO) Bw.Omar Jumanne Bakari
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Mkombozi Group (NGARABUTO) Bw.Amos Z.Mshina,kuhusu Usindikaji na Usambazaji wa Unga wa Muhugo katika maeneo ya Sengerema Mkoani Mwanza,wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa leo yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiangalia biashara mbali mbali ya mikoba wakati alipotembelea leo maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam,(kulia) Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa wote (EOTF) Mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa. Picha na Ikulu
  • Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiuliza swali kwa mjasiliamali wakati alipotembelea banda la wanawake Wajasiliamali (WIPE),
  • Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kuhusiana na uzazi wa mpango, wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE),

Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini akutana na Rais Dkt. Shein.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amekutana na Balozi wa Jamhuri ya Korea Mhe Song Geum-Young na kuzungumzia masuala mbalimbali ya uhusiano na ushirikiano.

Katika mazungumzo hayo Dk. Shein na balozi Young walisifu jitihada za serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Korea za kuimarisha uhusiano huo tangu nchi mbili hizo zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia miaka ya tisini. “Tumefanya jitihada kubwa za kuimarisha uhusiano wetu na matokeo yake sasa nchi zetu zinashirikiana kwa karibu katika mambo mbalimbali katika nyanja za kidiplomasia, uchumi na maendeleo” Dk. Shein alimueleza Balozi huyo.

Alifafanua kuwa ushirikiano katika biashara na uwekezaji, elimu, afya na kilimo ambayo ni kati ya maeneo yaliyowekewa mkazo katika ushirikiano ni maeneo muhimu kwa kuwa yanasaidia jitihada za kupunguza kiwango cha umasikini hivyo kujenga ustawi wa wananchi. Dk. Shein alibainisha kuwa chini ya uhusiano huo, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar ikiwemo imekuwa ikifaidika na misaada mbalimbali ambayo imekuwa chachu katika kuongeza kasi ya jitihada za wananchi wa Tanzania kujiletea maendeleo.

Katika mazungumzo hayo Dk. Shein aliishukuru Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Korea kwa misaada yake kwa Serikali na watu wa Zanzibar na kuutaja mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji kuwa moja ya matokeo makubwa ya ushirikiamo kati ya nchi hiyo na Zanzibar. “Kupitia mradi huu wa umwagiliaji, tunatarajia kutimiza lengo letu la muda mrefu la kujitegemea kwa chakula hivyo ni habari njema kwetu kuwa taratibu za kuanza utekelezaji wa mradi huu zitakamilika hivi karibuni” Dk. Shein alieleza.

Pamoja na mradi wa kilimo cha umwagiliaji, Jamhuri ya Korea kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (KOICA) inaisaidia pia Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Ulimwenguni (FAO) mradi wa ufugaji wa samaki wenye thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 3.4. Dk. Shein alitambua mchango wa shirika la kazi za kijamii la Korea la SAEMAUL ambalo alisema limekuwa likifanya kazi nzuri za kusaidia maendeleo ya jamii katika maeneo ya vijijini hapa Zanzibar.

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Korea alimueleza Dk. Shein kuwa nchi yake inaupa kipaumbele uhusiano wake na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ingependa kuona unaimarika siku hadi siku. Alifafanua kuwa ujumbe maalum wa nchi hiyo utakuja tena nchini mwezi Julai 2016 kwa mazungumzo zaidi ya ushirikiano baada ya mkutano kama huo wa ushirikiano uliofanyika mwezi Aprili mwaka huu.

Balozi Young alieleza kufurahishwa kwake kuona zaidi ya vijana 80 wa kujitolea wa Kikorea wanashiriki hutoa huduma za kijamii katika sehemu mbalimbali za Tanzania ikiwemo Zanzibar. Alieleza kitendo hicho kuwa ni kilelezo kingine cha kuonesha na kuimarisha urafiki mzuri uliopo kati ya nchi yake na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika mkutano huo Balozi Young alimhakikishia Dk. Shein kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza miradi yake ya maendeleo.

DKT SHEIN AKUTANA NA WAZIRI AUGUSTINO MAHIGA

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga baada ya mazungumzo yao leo alipofika Ikulu Mjini.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya mazungumzo yao,[Picha na Ikulu.]17/06/2016.

DKT. SHEIN AWAONGOZA VIONGOZI MBALIMBALI KATIKA DUA YA KUMUOMBEA MAREHEMU MZEE KARUME

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mara alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar katika Hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume .
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akijumuika na Viongozi na wananchi katika Hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  • Baadhi ya Wananchi wa Mjini na Mashamba waliojumika kwa pamoja katika Hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  • Baadhi ya Viongozi na Wananchi kwa pamoja wakiwa katika Hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  • Miongoni mwa Akinamama wakimuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume wakati wa Hitma iliyosomwa leo katika Osifi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Wananchi mbali mbali wa dini tofauti.
  • Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwana Mwema Shein (katikati) Mama Fatma Karume (wa pili kulia) pamoja na Wake wa Viongozi wakiwa katika Hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  • Wanafunzi wa Madrasa kutoka Vyuo mbali mbali na wananchi waliohudhuria katika Hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  • Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe,Amani Abeid Karume,(wa pili kushoto) Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Ali Hassan Mwinyi(wa pili kulia) Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania Mhe.Mohammed Gharib Bilali(kulia)kwa pamoja wakiitikia dua iliyoombwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheik Khamis Haji Khamis baada ya kumalizika kisomo cha Hitma ya dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  • Sheikh Hamid Masoud Jongo kutoka Jijini Dar es Salaam akitoa mawaidha baada ya Hitma ya dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka shada la mauwa katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume baada ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli,kuweka Shada la mauwa katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume baada ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  • Balozi Mdogo wa China Bwana Xie Yunliang akiwawakilisha Mabalozi wa Nchi mbali mbali katika kuweka shada la mauwa katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume baada ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  • Mjukuu wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Ahmed Amani Abeid Karume akichukua shada la mauwa kwaniaba ya wenzake kuliweka katika kaburi baada ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea Marehemu Babu yao, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli,(wa pili kulia) pamoja na Viongozi mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa.
  • Viongozi mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa.
  • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanawema Shein (kushoto) Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume,Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume,Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi pamoja wake wa Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akifuatana na wasaidizi wake akitoka eneo la kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume liliopo nje ya Jengo la Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar baada ya kumalizika hafla ya dua na uwekaji wa mashada ya mauwa iliyofanyika leo,na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono viongozi na wananchi walihudhuria katika hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika leo baada ya kumalizika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar na uwekaji wa mashada ya mauwa ambapo Viongozi na Wananchi mbali mbali walihudhuria
  • Wake wa Viongozi wakiwa nje ya Ofisi Kuu wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar baada ya kumalizika kwa hitma ya kumuombea dua Rais wa kwaanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeeid Amani Karume iliyofanyika leo. [Picha na Ikulu.]