RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametembelea eneo la Mpigaduri linalotarajiwa kujengwa bandari mpya pamoja na eneo la Kinazini linalotarajiwa kujengwa mji wa kisasa ikiwa ni miongoni mwa juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kukuza uchumi na kuimarisha maendeleo na ustawi wa jamii.
Akiwa amefuatana na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Rais Dk. Shein alifanya ziara hiyo fupi ya kutembelea maeneo hayo ambayo yametengwa maalum kwa miradi hiyo ya ujenzi wa bandari mpya pamoja na mji mpya wa kisasa.
Dk. Shein alitembelea maeneo hayo ambayo yametengwa maalum kwa miradi hiyo ambayo ujenzi wake ni miongoni mwa juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufungua milango zaidi ya kiuchumi sambamba na kuleta maendeleo endelevu kwa Zanzibar na wananchi wake.