Ikulu Blog

Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Mwinyi amezindua Filamu ya Tanzania Royal Tour leo Zanzibar.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhi Tuzo ya Muigizaji wa Filamu ya Tanzania Royal Tour na (kushoto kwa Rais) Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Utamaduni na Filamu Zanzibar (BASFU) Dkt. Omar Abdalla na (kulia kwa Rais)Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania.Dkt.Kiagho Kilonzo.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia Filamu ya Tanzania Royal Tour baada ya kuizindua katika ukumbi wa Hoteli ya Goldeg Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Jijini Zanzibar leo 7-5-2022 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwake) Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na wakiwa na Wake wa Viongozi wakifuatilia Filamu ya Tanzania Royal Tour, iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Jijini Zanzibar leo 7-5-2022.
  • WAGENI waalikwa na Wananchi wa Zanzibar wakifuatilia Filamu ya Tanzania Royal Tour, iliyozinduliwa leo 7-5-2022 Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Jijini Zanzibar.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia Uzinduzi wa Filamu ya Tanzania Royal Tour.(kulia kwake)Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Mgeni Hassan Juma, uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Unguja Jijini Zanzibar leo 7-5-2022, iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Filamu ya Tanzania Royal Tour, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Jijini Zanzibar leo 7-5-2022.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Filamu ya Tanzania Royal Tour, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Jijini Zanzibar leo 7-5-2022.
  • WAGENI waalikwa na Wananchi wa Zanzibar wakifuatilia Filamu ya Tanzania Royal Tour,iliyozinduliwa leo 7-5-2022 Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Jijini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na kuzungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Chakula Duniani Nchini Tanzania Bi.Sarah Gordon-Gibson Ikulu Zanzibar leo.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Nchini Tanzania Bi.Sarah Gordon-Gibson.(kulia kwa Rais) akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 5-5-2022.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Nchini Tanzania Bi.Sarah Gordon-Gibson, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 5-5-2022.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Nchini Tanzania Bi.Sarah Gordon-Gebson.(kulia kwa Rais) alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 5-5-2022.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Nchini Tanzania Bi.Sarah Gordon-Gibson.(kulia kwa Rais) akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 5-5-2022.

Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi ametowa Mkono wa Eid Fitry kwa Wananchi katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumaliza mazungumzo na Masheikh wa Zanzibar walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa kumsalimia leo 3-5-2022, baada ya kumaliza kwa Sala ya Eid Fitry iliyofanyika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja Jijini Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman, baada ya kumaliza mazungumzo yake na Masheikh wa Zanzibar Ikulu Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa Eid Fitry kwa Watoto waliofika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kupokea Mkono wa Eid Fitry, baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Masheikh wa Zanzibar, baada ya kumaliza Sala ya Eid Fitry iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja, mazungumzo hayo yaliofanyika Ikulu Jijini Zanzibar, walipofika kumsalimia leo 3-5-2022.

Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amelihutubia Baraza La Eid Fitry Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akipokea salamu ya heshima kutoka Kikosi cha Jeshi la Polisi cha FFU gwaride maalumu lilioandaliwa kwa ajili ya Baraza la Eid Fitry katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar.
  • BAADHI ya Mawaziri na Wageni waalikwa katika hafla ya Baraza la Eid Fitry wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akilihutubia katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akipokea salamu ya heshima kutoka Kikosi cha Jeshi la Polisi cha FFU gwaride maalumu lilioandaliwa kwa ajili ya Baraza la Eid Fitry katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja Jijini Zanzibar leo 3-5-2022.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia tafsiri ya maelezo mafupi ya Aya Suratul-Fat’hi wakati wa hafla ya Baraza la Eid Fitry lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Unguja na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.

Rais wa Zanzibar Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na waumini wa Dini ya Kiislam katika Sala ya Eid Elfity Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Sala ya Eid Fitry iliyofanyika leo asubuhi katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja Jijini Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Dini baada ya kuwasili katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja kuhudhuria Sala ya Eid Fitry baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Sala hiyo iliyofanyika katika Masjid hiyo leo 3-4-2022.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika viwanja vya Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja wakati ikipingwa mizinga baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid Fitry iliyofanyika katika Masjid hiyo na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.