Ikulu Blog

Dk.Shein ameongoza Wananchi katika Hitma ya Mzee Karume.

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, kuhudhuria hafla ya Hitma ya Dua ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
  • Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mkuu Brigedi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo,alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuhudhguria Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume
  • Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dkt. Amani Abeid Karume akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja akihudhuria hafla ya Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Viongozi na Wananchi katika Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi na Rasi Mstaaf wa Tanzania Mzee Aliu Hassan Mwinyi na kulia Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali,Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ameni Karume na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dr. Abdallah Juma Sadala.
  • Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ali akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud Mohammed alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuhudhuria hafla ya Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
  • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi wa Zanzibar katika Hitma na Dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, kushoto Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Mgeni Hassan Juma na kulia Mama Shadya Karume na Mama Fatma Karume,wakiitiikia dua wakati wa hafla hiyo ya Hitma ya Mzee Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika leo Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
  • WANANCHI kutoka sehemu mbalimbali ya Mji wa Zanzibar wakihudhuria Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.(
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua ya kuhitimisha Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ,ikisomwa na Sheikh Jaffar Abdallah Abdald, katika hafla hiyo iliofanyika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Salif Omar Kabi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seiff Ali Iddi na Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi na kulia Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali nac Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Dkt Amani Abeid Karume
  • WANAINCHI wakishiriki katika Kisoma cha Hitma ba Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
  • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuhudhuria Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume
  • MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika kaburi la Mareheme Mzee Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika dua ya kumuombea iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar
  • MWAKILISHI wa Familia ya Marehemun Mzee Abeid Amani Karume,Balozi Ali Karume baada ya kumalizika hafla ya kisomo cha Hitma na Dua kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibaer
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka Shada la Maua katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika kwa kisomo cha Hitma iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ungyuja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud na kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakitoka katika viwanja vya Kaburi la Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika kwa dua na kuweka mashada ya mau.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapiunduzi Mhe,.Dk. Aliu Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, katika kamuri la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Rais wa Kwa wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Afisiu Kuu ya CCM Zanzibar
  • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akijumuika katika dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, kulia Mjane wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Mama Fatma Karume na Mama Shadya Karume wakiitikia dua wakiwa katika viwanja vya karubi katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ungyuja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud na kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakitoka katika viwanja vya Kaburi la Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika kwa dua na kuweka mashada ya mau.
  • WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Januari Yussuf Makamba baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kumuombea Dua Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar

Dk.Shein Azungumza na Executive Coordinotor wa Program ya Kujitolea ya “United Nations Volunteers”

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mratibu Mkuu wa Program ya Kujitolea ya "United Nations Volunteers " (UNV) Bw,Oliver Adam kushoto,alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Mhe Rais
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mratibu Mkuu wa Programu ya Kujitolea ya (UNV) " United Nations Volunteers "Bw.Oliver Adam, kushoto akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mratibu Mkuu wa Programu ya Kujitolea ya (UNV) " United Nations Volunteers "Bw.Oliver Adam, kushoto akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Zanzibar leo kwa mazungumzo.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mratibu Mkuu wa Program ya Kujitolea yaRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mratibu Mkuu wa Program ya Kujitolea ya "United Nations Volunteers " (UNV) Bw,Oliver Adam.

Dk.Shein: Watu hawaziheshimu na hawazifuati sheria za ardhi

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa Semina ya Kitaifa Kuhusiana na Masuala ya Ardhi na Rasilimali zisizorejesheka Zanzibar, ikiwashirikisha Wadau wa Ardhi na Sheria , inliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni
  • WAZIRI wa Ardhi Maji Nyumba na Nishati Mhe. Salama Aboud Talib, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindsuzi Mhe,. Dk.Ali Mohamed Shein, kufungua Semina hiyo ya Siku moja kwa Watendaji wa Serikali iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil kikwajuni Zanzibar.
  • MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Mhe. Said Hassan Said, akisoma kabrasha wakati wa hafla ya Semina ya Kitaifa ya Kuhusiana na Ardhi na Rasilimali Zisizorejesheka Zanzibar, iliofanyika katika Ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, akiwa na Waheshimiwa Majaji wa Mahkama Kuu Zanzibar.
  • BAADHI ya Washiriki wa Semina ya Kitaifa ya Kuhusiana na Masuala ya Ardhi na Rasilimali Zisizorejesheka Zanzibar, wakifuatilia hafla hiyo katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa Semina ya Kitaifa Kuhusiana na Masuala ya Ardhi na Rasilimali zisizorejesheka Zanzibar, ikiwashirikisha Wadau wa Ardhi na Sheria , inliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni
  • NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatilia semina hiyo wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein akihutubia wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo iliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
  • BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kulia Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe. Mmanga Mjawiri , Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar,Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa, Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe. Balozi Amina Salum Ali na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar. Mhe. Haroun Ali Suleiman, wakifuatilia hutuba ya Ufunguzi wa Semina ya Kitaifa ya Kuhusu Masuala ya Ardhi na Rasilimali Zizisorejesheka Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni.
  • MRAJISI wa Ardhi Wizara ya Ardhi,Nyumba Maji na Nishati Zanzibar Dkt. Abdul-Nassir Hemed Hikmany, akiwasilisha Mada kuhusiana na Matumizi ya Ardhi Zanzibar, wakati wa hafla ya Semina hiyo iliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
  • WAZIRI wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed, akichangia Mada iliowasilishwa kuhusu Matumizi ya Ardhi Zanzibar wakati wa Semina hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
  • JAJI wa Mahkama Kuu Zanzibar Mhe. Rabia Mohammed, akichangia wakati wa Semina hiyo iliowashirikisha Wadau mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuzungumzia Matumizi ya Ardhi Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrissa Abdulwakil kikwajuni Zanzibar.
  • WAZIRI Asiyekuwa na Wizara Maalum (MBM) Mhe. Said Soud akichangia Mada wakati wa Semina ya Kitaifa Kuhusu Masuala ya Ardhi na Rasilimali zisizorejesheka Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
  • MWENYEKITI wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Jaji Mshibe Ali Bakari, akichangia Mada wakati wa Semina ya Kitaifa Kuhusu Masuala ya Ardhi na Rasilimali Zisizorejesheka Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni.
  • KATIBU Mtendaji wa Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Sheikh.Abdallah Talib, akichangia Mada kuhusiana na Matumizi ya Ardhi wakati wa semina hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil kikwajuni Zanzibar.

Dk.Shein amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Ndg. Khalid Abdallah Omar.RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Ndg. Khalid Abdallah Omar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali kushoto Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid,Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja.Bi. Hamida Mussa Khamis na Naibyu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Ndg Khalid Abdallah Omar na kulia Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Said Hassan Said,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Saleh Kabi na Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg.Omar Said Ameir.
  • BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakihudhuria hafla ya kuapishwa Viongiozi walioteuliwa hivi karibuni, kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Saleh Kabi
  • BAADHI ya Wanafamilia wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakihudhuria hiyo ya kuapisha iliofanyika Ikulu Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimpongeza Naibu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Ndg. Khalid Abdallah Omar, wakati wa hafla hiyo iliofanyika Ikulu Zanzibar
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Bi. Hamida Mussa Khamis, hafla hiyo imefanyika 13-3-2019, Ikulu Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Ndg. Khalid Abdallah Omar, hafla hiyo imefanyika 13-3-2019, katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg. Omar Said Ameir, hafla hiyo imefanyika 13-3-2019
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisaini hati ya Kiapo ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg. Omar Said Ameir, hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar.

Mama Mwanamwema Shein mgeni rasmin siku ya Wanawake Gombani Pemba.

  • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania.(UWT) Bi.Gaudensia Kabaka,alipowasili katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba, kuhudhuria Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa zimefanyika Kisiwani Pemba katika Uwanja wa Gombani 8-3-2019.
  • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akitembelea Maonesho ya Wajasiriamali Wanawake Kisiwani Pemba yaliofanyika katika viwanja vya Gombani chakechake, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi.
  • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiangalia Bidhaa za Wajasiriamali Wanawake wa Kisiwani Pemba wakati akitembelea maonesho hayo ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika Kisiwani Pemba Uwanja wa Gombani, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama.Asha Suleiman Iddi.
  • Wanawake kutoka sehemu mbali mbali Kisiwani Pemba wakifuatilia hutuba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akihutuba wakati wa hafla hiyo ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Pemba 8-3-2019.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,akiwasalimia Vijana wa Madrasa kutoka Chake Chake wakipiga dufu,wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika Kisiwani Pemba katika Uwanja wa Gombani.
  • Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akihutubia wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika Kitaifa Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba,8-3-2019.