Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 2 Oktoba, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Ashatu Kachambwa Kijaji aliyefika Ikulu, Zanzibar kujitambulisha rasmi.

Mhe Rais amempongeza Waziri Dk. Kijaji kwa kuendeleza ushirikiano kati ya Wizara hiyo na Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano ya Zanzibar. Aidha Rais Dk. Mwinyi amesisitiza haja ya kuendelezwa ushirikiano kati ya Wizara mbili hizo na kusema ana matumaini makubwa mafanikio zaidi yataendelea kupatikana kwa azma ile ile ya kuiletea maendeleo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwa upande wake Waziri Dk. Ashatu Kijaji aliyeongozana na ujumbe wa Wizara yake akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Zainab Chaula amemshukuru Mhe. Rais Dk Mwinyi na kuahidi kufanyia kazi maelekezo na ushauri alioutoa kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.