Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za pole kwa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Saba Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha Kaka yake Mzee Shein Mohamed Shein kilichotokea jana (Novemba 14,2021).

Katika salamu hizo za pole,  Rais Dk. Mwinyi alieleza kusikitishwa kwake na kifo hicho na kumtakia pole na ustahamilivu Rais Mstaafu Dk. Shein yeye na familia yake katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Rais Dk. Mwinyi na familia yake wamemuomba Mwenyezi Mungu amjaalie Marehemu Mzee Shein Mohamed Shein amlaze mahala pema peponi, Amin.

Rais Dk. Mwinyi ametoa salamu hizo akiwa Jijini Durban, nchini Afrika Kusini akisihiri ufunguzi wa Mkutano wa Maonyesho ya Kukuza Biashara baina ya nchi za Afrika.