KIKAO cha Kamati Kuu (CCM) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimefanyika leo kikiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma ambacho kilihudhuriwa na viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya (CCM). Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Kikao hicho ambacho ni cha kawaida na cha kwanza kwa Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo kimefanyika kujadili masuala mbali mbali ya chama hicho cha CCM.Kikao hicho kimefanyika baada ya Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika jana Juni 21,2021 chini ya Mwenyekiti wake Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo huko katika ukumbi wa NEC, White House Jijini Dodoma.