RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewapisha Washauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliowateua hivi karibuni.

Walioapishwa ni Bwana Abdalla Rashid Abdalla aliyeapishwa kuwa Mshauri wa Rais Mambo ya Siasa.

Aidha, Dk. Shein amemuapisha Bwana Ali Mzee Ali kuwa Mshauri wa Rais katika Masuala ya Historia na Mambo ya Kale.

Hafla ya kuwapishwa viongozi hao ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na Makatibu Wakuu. 

Wengine ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu Kadhi wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Viongozi wa Vikosi vya SMZ, Washauri wa Rais wa Zanzibar, viongozi wengine wa Serikali pamoja na wanafamilia.

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo Bw.Ali Mzee Ali baada ya kuapisha kuwa mshauri wa Rais katika masuala ya Historia na Mambo ya Kale katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar