Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar ambapo pia, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee walishiriki.
Akisoma Taafira ya utangulizi ya utekelezaji wa Malengo makuu hayo ya Wizara, Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nassor Ahmed Mazrui alisema kuwa hata hivyo, Wizara inafuatilia kwa karibu zaidi mwendendo wa upatikanaji chakula duniani kutokana na upungufu wa mavuno hasa ngano katika nchi zinazozalisha zao hilo kwa wingi.Alizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na Marekani, Australia na Urusi ambazo zimekumbwa na ukame mkubwa katika msimu uliopita na kukiri kuwa upungufu wa uzalishaji unaweza kuwa na athari katika soko la zao hilo duniani.Aidha,Uongozi huo ulieleza kuwa katika kipindi cha robo ya nne ya bajeti ya 2011/2012 na kipindi cha robo ya kwanza ya bajeti ya 2012/2013 wastani wa mwenendo wa bei za chakula muhimu katika soko la dunia ziliendelea kuwa za utulivu.
Uongozi huo ulieleza kuwa kwa upande wa mwenendo wa bei za bidhaa za mchele, sukari na unga wa ngano kwa soko la ndani, uliendelea kuwa na utulivu ikilinganishwa na nchi jirani na hata Tanzania Bara.Kwa maelezo ya Wizara hiyo, mwenendo huo wa utulivu umetokana na mchanganyiko wa hatua za kisera zinazochukuliwa na Serikali katika kutuliza makali ya hali ya maisha kwa wananchi wake.
Kwa upande wa uvunaji na biashara ya Karafuu, Wizara hiyo ilieleza kuwa msimu wa uvunaji karafuu ulitangazwa rasmi tarehe 07 Agosti, 2012 ambapo ununuzi ulianza na hadi tarehe 4 Disemba, 2012 jumla ya tani 164.4 zilinunuliwa kwa thamani ya TSh. 1,967.2 kutoka kwa wakulima.
“Ikilinganishwa na mwenedo wa ununuzi kwa msimu uliopita kasi ya ununuzi msimu huu ni ndogo”,ilieelza Wizara hiyo.Aidha, Wizara hiyo ilieleza kuwa kwa upande wa bei ya kununulia kutoka kwa wakulima ilifikia TSh. 12,500 kwa kilo kutoka TSh. 10,000 iliyotangazwa wakati wa ufunguzi wa msimu ambapo ongezeko hilo linatokana na kuimarika kwa soko la karafuu ilinalotokana na kupanda kwa mahitaji duniani na hasa Indonesia na India.
Pia, Wizara hiyo ilieleza kuwa ili kujiendeleza katika uwekaji wa misingi mizuri ya kustawisha viwanda, iliendelea na utekelezaji wa hatua za utayarishaji wa Sera mpya ya Viwanda hatua kwa hatua na pia, kuwendelea na mazingatio ya ndani ya utafiti wa kuifanya Zanzibar kuwa eneo tengefu la kiuchumi.
Wizara ilieleza kuwa hatua mbali mbali zimeendelea kuchukuliwa kwa lengo la kukuza na kutafuta fursa za kimasoko kwa kutumia njia za maonesho, majadiliano ya kibiashara katika ngazi ya kanda na kimataifa na hata ushirikiano wa nchi na nchi.Hivi sasa pia, Wizara inaendelea na hatua za kuweka misingi ya kisheria kuhusu biashara, mfumo wa leseni za biashara, mifumo ya ushindani na vipimo, viwango vya bidhaa na taasisi zake. Pia iliahidi kuzilinda bidhaa za viungo vya Zanzibar ili kuongezwa thamani zikiwemo karafuu, mdalasini, hiliki, tangawizi na pilipilimanga.
Kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, uongozi huo ulieleza kuwa Wizara hiyo inaendelea na mpango wa kupanda miche mipya ya mikarafuu Unguja na Pemba.
Nae Dk. Shein aliipongeza Wizara hiyo kwa juhudi zake katika kuhakikisha inafanikisha malengo yake na kusisitiza kuwa taarifa ya mwenendo wa hali ya chakula inatia moyo sana hivyo juhudi zinatakiwa kuendelezwa ili mafabnikio zaidi yaweze kupatikana.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa hatua zilizofikiwa katika uvunaji na biashara ya karafuu nazo pia, zinatia moyo hivyo kuna haja ya kuongeza bidii ili ziweze kuimarika zaidi na kuleta tija katika kuimarisha uchumi nchini.