RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha George Joseph Kazi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Hafla ya kuapishwa kiongozi huyo ilifanyika Ikulu Jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi Gavu, Waziri wa Katiba na Sheria Khamis Juma Mwalimu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na Makatibu Wakuu. 

Wengine ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan, Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Saleh Juma Kinana , Washauri wa Rais wa Zanzibar,  Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mawakili,  viongozi wengine wa Serikali pamoja na wanafamilia.