RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Mapinduzi yalikuwa ni lazima yatokee na kufanywa kutokana na dhulma zilizokuwepo hapa Zanzibar kutokana na utwala wa Kigeni wa Kisultani na Kiengereza na ndipo vuvuguvugu la Mapinduzi likaanza.Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya ufunguzi wa Daraja la Kimbonde Mzungu, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, hafla iliyofanyika katika eneo hilo la Kibonde Mzungu ikiwa ni shamrashamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.Katika hafla hiyo Rais Dk. Shein alieleza kwa ufupi historia ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na kueleza juhudi zilizochukuliwa katika kuhakikisha wanyonge wa Zanzibar wanakuwa huru.
Rais Dk. Shein alisema kuwa Mapinduzi yatasemwa kila siku kwani ni jambo ambalo lina maslahi ya wananchi wote kwani kuna baadhi ya watu hawapendi kuyataja na kuyazungumza Mapinduzi.Alisema kuwa Mapinduzi yalikuwa ni lazima yatokee na kufanywa kutokana na dhulma zilizokuwepo hapa Zanzibar kutokana na utwala wa Kigeni wa Kisultani na Kiengereza na ndipo vuvuguvugu la Mapinduzi likaanza.Alisema kuwa uchumi wa Zanzibar waliuhodhi, elimu, afya na kila kitu na mnyonge alikuwa hana maana wala starehe za aina yotote na badala yake kulikuwa na mipaka na mahala pa kushereheka na muda pamoja na saa maalum za kufanya starehe.
Pia, alisema kuwa Mapinduzi ya Januari 12, 1964 nchi zote duniani ziliyatambua hasa kwa malengo yake ya kujenga umoja wa watu wa Zanzibar, kujenga mshikamano na maelewano, amani sambamba na kuondosha ubaguzi na kutunga Sheria ya mwanzo ya Rais, Sheria Namba 6, iliyotiwa saini mnamo tarehe 25 Februari 1964.Alisema kuwa katika uongozi wa Rais Karume kila kitu kiliongozwa kwa sheria na taratibu za nchi zilizopo.Rais Dk. Shein alisema kuwa ujenzi wa barabara na daraja hilo ni uthibitisho wa matunda ya Mapinduzi kwani kabla ya Mapinduzi hapakuwepo madaraja na barabara nzuri kama zinazojengwa hivi sasa.
“tingatinga ndio daraja kubwa lililokuwepo wakati huo lililojengwa na Wajerumani ambayo hayakuwa madaraja wala barabara zilizokuwa kubwa ili wanananchi waizutumie wka ajili ya kusarifi wao na bidhaa zao.
Alisema kwua baada ya Mapinduzi ndio kila kiyum kilishamiri zikiwemo ujenzi wa barabara , nyumba na mambo mengimen., “tunachokitaka wenyewe tunajenga, na mimi nataka nikukumbusheni mwaka 2017”,.
“Tujengeni daraja kubwa la kisasa hapa, daraja liwepo tena liwe kuwab na zuri”.Alisema kuwa Setikali iliamua kwani inajengwa kwao na ni jukumu lake la kuwajengewa wananchi wote wanaokwenda kwa mifuuu na wanaotumia usafiri wa aina zote.Alisema kuwa wakoloni hawakujenga kwani tokea wakati huo Kimbonde Mzungu ilikuwepo na wao walikuwa na habari ya Mji Mkongwe na Mjini. Walidiriki kujenga treni katika eneo la mjini pekee.
Ndani ya miaka 56, kumefanywa mamapnbo mengi na Zanzibar sivyo ilivyokuwa wakati huo ikilinganishwa na hivi sasa.Kila fedha inaporuhusu, tutajenga barabara hata barabara za juu (Flaiover), Kinazinni, Bububu hadi Mahonda, kwani gari ni nyingi sana.Lazima Serikali ianze utaratibu wa jkunenga barabara, na ndipo uwamuzi ama njia ya kuvunja nyumba ili kujenga nyumba.Tayari ameshatoa agizo kwa Wizara ya Mawasiliano kutafuta jibu la ujenzi wa barabara ya juu kuelekea Kaskazini iaze wapi kwani ni lazima Serikali ifanye.
UJENZI WA Daraja Kibonge Mzungu ni Mapinduzi kwani ni kufanya jambo ambalo linatakiwa na wananchi.Alsiema kwua Mapindhzia yamefanwya na watu wanaendelezwa na watu na yatadumishwa na watu. Aliwataka Wizara kuhakikisha mjenzi anayejenga hadi Febuari anakabidhi barabara na kutaka mkataba usivukwe.
UUB watajenga wakaunganishe barabara inayoelekea Koani, wakwani wana vifaa vipya, wataalamu wanao na basi tena kutoa tenda kwa lile eneo linalowezekana.Haiwezekani kununua vifaa vya Bilioni 14 halafu wakaanza kutoa tenda na kuwataka kujenga wenyewe Pemba na Unguja na ile kubwa watoe tenda lakini kwa ile wanayoweza wafanye wenywe wasipigwe dongo la macho.Tunauwezo wa kujenga tujenge wenyewe, na nawawataka kutokunja mikono kwani wananchi watawaudhi kwani ndio wenye nchi yao na fedha zao.Mtambo wa kisasa mpya kutoka Brazil na vifaa vyengine vipya huku akisisitiza kwua mammbo ya msingi yawe msingi.Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein amekubali Daraja hilo kuitwa jina lake na kupokea heshima hiyo na kumpongeza Wzari, katibu Mkuu na wafanyakazi wote wa Wizara hiyo kwa kushirikiana na mkandarasi.
Alieleza haja ya kutiwa taa za barabarani kuanzia Jumbi bango la Mkoa hadi kituo cha Polisi cha Fuoni kuwekwa taa jambo ambalo limeunwga mkono na Wizara husika kwani hayo ni maendeleo kwani barabara kutiwa taa ni jambo muhimu sambamba na kujenga mitaro pembezoni mwa barabara.
Nae Waziri wa Mawasiliano .... Dk. Sira Ubwa Mwamboya alisema kuwa,Ilikuwa ni changamoto kubwa sana hasa wakati wa mvua na maji yalikuwa yanajaa na kusababisha madhara ambapowka sasa tatuzo hilo limeondka na litakuwa ni historia na wananhi hivi sasa wanapita usiku na mchana.Katika maelezo Ni utekelezajiw a Ilani ya Uchgauzi ya CCM, juhudi zimefanywa katika… madaraja yote yatafanyiwa kazi ambayo yamepata athari katika mvua zilizopifta.
Waziri huyo alimpongeza Rais Dk. Shein kwa miongozo yake na kumuhakikishia kuwa watafanya kazi kwa kadri ya uwezo wao katika kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo hasa katika sekta ya usafiri.Waziri Sira aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa Mfuko wa Barabara kwa juhudi kubwa zilizochukuliwa katika kuhakikisha daraja hilo linajengwa na barabara hiyo nayo inajengwa na kupitika tena kwa kiwango kizuri na kuwapongeza wale wote waliofanikisha ujenzi huo na kuwaomba wananchi wote wa Unguja na Pemba kuzitunza barabara kwani zinagharimu fedha nyingi katika ujenzi wake.
Alisema kuwa barabara zinagharimu fedha nyingi hasa pale zinapoharibika kwa bahati mbaya ama pale zinapoharibiwa kwa makusudi,sambamba na hayo, Waziri Dk. Sira alisisitiza haja ya kuyaenzi, kuyalinda na kuyadumisha Mapinduzi ya Januari 12, 1964 kwani ndio ndira yetu ya maendeleo hapa nchini.Hata hivyo, Waziri Dk. Sira alimuomba Rais Dk. Shein kuwa daraja hilo liiitwe kwa jina lake Rais Dk. Shein ili iwe kumbukumbu ya wananchi kutokana na juhudi zake alizozichukua katika kuhakikisha tatizo la Daraja hilo linapatiwa ufumbuzi na wananchi wanapita wakati wote.