Hafla hiyo ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis.
Wengine waliohudhuria katika hafla hiyo ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib, Washauri wa Rais pamoja na viongozi wengine wa Serikali