Media » News and Events

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameivunja Bodi ya Kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameivunja Bodi ya Kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO) kuanzia leo tarehe 20 Agosti, 2021.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mussa Haji Ali, Mhe. Rais Dk. Mwinyi ameivunja Bodi hiyo iliyoanza majukumu yake tarehe 9 Juni 2017.

Zanzibar Fisheries Company Ltd (ZAFICO) ni Kampuni ya Uvuvi Zanzibar iliyoanzishwa na kuanza kazi mnamo Oktoba 2017. Kampuni hiyo iko chini ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi

Download File: