Kwa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 6(1)(a) cha Sheria ya mambo ya Rais nambari 3 ya mwaka 2020 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Ali Mohamed Shein ametangaza kwamba siku ya Jumatatu Tarehe 02 Novemba,2020 itakuwa siku ya Mapumziko ili kutoa fursa kwa watumishi wa umma na wananchi kuhudhuria za kuapishwa kwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.