Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi kwa viongozi katika taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

1. Bwana Hassan Khatib Hassan ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini na Magharibi.

2. Bwana Ayoub Mohammed Mahmoud ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.

3. Dkt. Iddi Hussein Hassan ameteuliwa kuwa katibu mtendeji wa kamisheni ya Ardhi na Mazingira.

4. Bwana Ahmed Abdulrahman Rashid ameteuliwa kuwa Mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa Barabara.

5. Bwana Said Salmin Ufuzo ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Jiji la Zanzibar anaeshughulikia masuala ya mipango miji.

6. Kapteni Juma Hussein Ali ameteuliwa Mkuu wa Utawala katika kikosi cha Valantia (KVZ).

7. Bwana Asaa Ahmad Rashid ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Bandari la Zanzibar.

8. Bwana Louis Henry Majaaliwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Utumishi ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 18 Septemba, 2019