Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 94(2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana George Joseph Kazi kuwa JAJI WA MAHKAMA KUU YA ZANZIBAR.

Uteuzi huo unaanzia leo tarehe 17 Septemba, 2020.