Dk. Shein aliyasema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na Shirika la Utangazi la Zanzibar kupitia televisheni,  ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu mjini Zanzibar.Dk. Shein alisisitiza kuwa zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa lisihushishwe na mambo ya siasa kwani hilo ni jambo la serikali na kuwataka viongozi wote katika jamii wakiwemo viongozi wa kisiasa kushirikiana pamoja katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.Alisema kuwa kufanikiwa kwa zoezi hilo kutawapelekea wananchi kupata vitambulisho vyao vya Taifa ambavyo vitawawezesha kujilabu kuwa wao ni Watanzania.“Wanananchi msihadaiwe wala msidangaywe na mtu yoyote kwani vitambulisho hivyo vitakusaidieni kukutambulisheni Utanzania wenu”,alisema Dk. Shein.Dk. Shein alisema kuwa hiyo ni fursa ya pekee na ana amini kuwa wananchi wote watajitokeza kwa wingi ili kupata haki yao hiyo ya msingi kwa lengo la kupata tija katika maendeleo yao na faida kwao na nchi nzima kwa ujumla.
Aidha, alitoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuwaelimisha wananchi kujua umuhimu wa Vitambulisho hivyo huku akiwataka kuwasisitiza kujitokeza kwa wingi kutokana na umuhimu wake mkubwa katika maendeleo ya Mtanzania.Dk. Shein pia, aliwataka viongozi wa dini wakiwemo Mashekhe na Maaskofu kujitahidi katika kuwaeleza waumini wao juu ya umuhimu wa kujiadikisha kwa kupata vitambulishio hivyo vya Uraia.