Katika mazungumzo hayo Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa Zanzibar ina mengi ya kujifunza kutoka Vietnam kutokana na nchi hiyo kupata mafanikio makubwa katika uimarishaji wake wa uchumi na pamoja na sekta za maendeleo.Dk. Shein alisema kuwa miongoni mwa maeneo muhimu ya kuimarisha zaidi ushirikiano huo kati ya Zazibar na Vietnam ni pamoja na sekta ya uvuvi, kilimo, utalii, uimarishaji wananchi kiuchumi, biashara pamoja na sekta nyenginezo.Aidha, Dk. Shein amueleza Makamu huyo wa Rais kuwa Tanzania na Vietnam zimekuwa na uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu tokea miaka ya 1960 na zimeweza kuungana mkono katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo, kiuchumi na hata kisiasa.
Dk. Shein alimueleza kingozi huyo hatua zinazochukuliiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeleo na uchumi na mafanikio yaliofikiwa katika kutekeleza Dira ya 2020 pamoja na Mkakati wa Kukuza Uchumi a Kupunguza Umasikini (MKUZA).
Kwa upande wa kilimo Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa Tanzania imeweka mikakati maalum ya kuimarisha sekta ya kilimo ambapo kwa upande wa Zanzibar Serikali mechukua juhudi kubwa katika kuhakikisha sekta hiyo inapewa kipaumbele.Dk. Shei alisema kuwa sekta ya kilimo ndio uti wa mgongo wa Zazibar hali ambayo inapelekea kutafuta kila njia katika kuhakikisha sekta hiyo inaimarika ikiwa ni pamoja na kuimarisha kilimo cha kisasa chenye kuendana na sayansi na tekolojia na kuwapa unafuu wakulima wadogo wadogo kwa kuwawekea mazingira bora ya kilimo.Mbali ya juhudi hizo, Dk. Shein alimueleza kionhozi huyo hatua zilizochukuliwa na Serikali yake katika sekta ya kilimo kwa kukimarisha Chuo cha Utafiti wa Kilimo kiopo Kizimbani Zanzibar kusisitiza haja ya kuwepo mashirikiano katika utafiti huo wa kilimo.