YALIYOMO
1. ORODHA YA VIAMBATISHO ................................................................................................................................................................................................................................ iii
2. VIFUPISHO VYA MANENO .................................................................................................................................................................................................................................. iv
3. UTANGULIZI ........................................................................................................................................................................................................................................................ 1
4. MAJUKUMU YA AFISI YA RAIS IKULU .................................................................................................................................................................................................................. 3
5 MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA AFISI YA RAIS IKULU KWA KIPINDI CHA JULAI – MACHI 2021/2022 .......................................................................................... 7
6. MWELEKEO WA BAJETI YA AFISI YA RAIS IKULU KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023 .................................................................................................................................... 39
7. PROGRAMU KUU NA NDOGO NA MAKISIO YA FEDHA ZINAZOHITAJIKA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023 ................................................................................................... 40
8. MAMBO MAKUU YATAKAYOTEKELEZWA NA AFISI YA RAIS IKULU KWA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA WA 2022/2023 .....................................................50
9. MAOMBI YA FEDHA KWA KAZI ZILIZOPANGWA KUTEKELEZWA KATIKA MWAKA WA FEDHA 2022/2023 ........................................................................................................... 50
10. HITIMISHO ....................................................................................................................................................................................................................................................... 51

BAJETI IKULU
iii ORODHA YA VIAMBATISHO
Kiambatisho Nam.1. Mchanganuo wa Maagizo kwa kila Mkoa. .................................................................................................................................................................................. 53
Kiambatisho Nam. 2. Orodha ya Mada zilizojadiliwa kupitia Televisheni na Redio katika kipindi cha “Unatekelezaje? kwa kipindi cha Julai 2021 - Machi 2022..............................................54
Kiambatisho Nam. 3. Idadi ya taarifa zilizorushwa na waliotembelea Tovuti ya Ikulu kwa Kipindi cha Miezi Tisa 2021 – 2022 ............................................................................................60
Kiambatisho Nam. 4. Taarifa zilizorushwa Kupitia Mitandao ya Kijamii ya Ikulu kwa Kipindi cha Miezi Tisa 2021 – 022.....................................................................................................61
Kiambatisho Nam. 5. Orodha ya Malalamiko yaliyowasilishwa na Wananchi kwa Kipindi cha Miezi 9 kutoka Julai mpaka Machi 2021/2022. .................................................................... 63
Kiambatisho Nam. 6. Takwimu za Malalamiko yaliyowasilishwa na Wananchi kwa Taasisi 45 za Serikali zilizounganishwa katika Mfumo wa Sema na Rais kwa Kipindi Julai – Machi 2021/2022. .............................................................................................................................................................................................................................................................64
Kiambatisho Nam. 7. Idadi ya Taasisi na Watumishi waliopatiwa Semina ya Utunzaji Nyaraka na Udhibiti wa Siri za Serikali........................................................................................... 68
Kiambatisho Nam. 8. Mapitio ya Utekelezaji wa Bajeti ya Kazi za Kawaida kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 na Makadirio ya Bajeti ya Mwaka 2022/2023. ...............................................69

BAJETI IKULU
iv VIFUPISHO VYA MANENO
AfCFTA Afirca Continental Free Trade Area (Soko huru la Biashara la Nchi za Afrika)
AMREF African Medical and Research Foundation (Shirika la Utafiti wa Madawa Afrika)
AU African Union (Umoja wa Nchi za Afrika)
BLM Baraza la Mapinduzi
CCM Chama Cha Mapinduzi
COMESA Common Market for Eastern and Southern
Africa (Soko la Pamoja za Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika)
DRC Democratic Repulic of Congo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo)
EAC East Africa Community (Jumuiya ya Afrika Mashariki)
GSO Government Security Office (Afisi ya Usalama wa Serikali)
IORA Indian Ocean Rim Association (Jumuiya za Nchi zilizopakana na Bahari ya Hindi)
JCC Joint Commission for Cooperation (Tume ya Pamoja ya Ushirikiano)
JPC Joint Permanent Commission (Tume za Kudumu za Pamoja)
KBLM/KMK Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi
NTB’s Non-Tariff Barriers (Vikwazo vya Biashara Visivyo vya Kiushuru)
SADC Southern Africa Development Community (Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika)
SDG’s Sustainable Development Goals (Malengo ya Maendeleo ya Melenia)
BAJETI IKULU
v SMT Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
SMZ Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
SNR Sema na Rais
TEHAMA Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
TZS Tanzania Shiling (Shilingi ya Kitanzania
UAE United Arab Emirates (Umoja wa Falme za Kiarabu)
UNDP United Nations Development Programme
UNICEF United Nations International Children’s
Emergency Fund (Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto)
USD United State Dollar (Fedha ya Marekani)
UWEMAJO Umoja wa Wenye Mashamba Jozani
VVU/UKIMWI Ukosefu wa Kinga Mwilini
ZADEP Zanzibar Development Plan 2021 - 2026 (Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar)
ZAWA Zanzibar Water Authority (Mamlaka ya Maji Zanzibar)
ZBC Zanzibar Broadcasting Cooperation (Shirika la Utangazaji la Zanzibar)
ZCTV Zanzibar Cable Television
BAJETI IKULU

1 UTANGULIZI
1.Mheshimiwa Spika, naanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema kwa kutujaalia uzima na afya njema na kuweza kukutana hapa katika kikao hiki muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu. Aidha, kwa namna ya pekee namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuniamini na kuniteua kwa mara nyengine tena na kunipa jukumu la kuhudumu katika Afisi yake. Vile vile, nachukua fursa hii adhimu kumpongeza Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kutuongoza, kutuelekeza na kusimamia ipasavyo utekelezaji wa majukumu ya Serikali kama ilivyoainishwa katika Katiba, Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025, Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar 2021-2026 (ZADEP) na Mipango mikuu ya Maendeleo kwa Taifa letu.

2. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi anavyoiongoza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa weledi na kusimamia vyema Miradi mikubwa ya kimkakati katika kipinbdi cha mwaka mmoja cha uongozi wake.Aidha sisi sote ni mashahidi tunaona namna anavyoifungua nchi katika diplomasia ya uchumi.

BAJETI IKULU
2
3. Mheshimiwa Spika, nachukua nafasi hii kuwapongeza Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais na Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla, Makamu wa Pili wa Rais kwa namna ambavyo wanamsaidia Mheshimiwa Rais katika kutekeleza majuku yake ya kila siku ya kuongoza na kusimamia shughuli za serikali.
4. Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kukupongeza wewe binafsi, Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid na naibu wako Mheshimiwa Mgeni Hassan Juma na Mwenyekiti wa Baraza lako Tukufu Mheshimiwa Mwanaasha Khamis Juma kwa kuliongoza vyema Taifa hili. Katika uongozi wako tumeshuhudia uendeshaji wa mijadala iliyo wazi na yenye nidhamu ya hali ya juu ya waheshimiwa wajumbe wa Baraza lako.
5. Mheshimiwa Spika, natoa shukran maalum kwa Mwenyekiti wa kamati ya kusimamia Afisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa, Mheshimiwa Machano Othman Said Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini na Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Mtumwa Peya Yussuf, Mwakilishi wa Jimbo la Bumbwini pamoja na Wajumbe wote wa Kamati kwa mashirikiano na miongozo wanayotupatia.
6. Mheshimiwa Spika, Afisi ya Rais Ikulu imeanzishwa kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa Mheshimiwa Rais katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu namba 50(04). Afisi ya Rais Ikulu ni matokeo ya mabadiliko ya Miundo ya

BAJETI IKULU
3 Wizara yaliyofanyika mara tu baada ya kuanza kwa Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Awali Afisi hii ilikuwa ni sehemu ya Afisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji na mnamo tarehe 10 Julai, 2021 ilianzishwa Afisi ya Rais Ikulu.
7. Mheshimiwa Spika, Afisi ya Rais Ikulu katika Awamu hii ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeundwa upya na kuongezewa majukumu ya kushughulikia Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar. Kwa sasa, Afisi ya Rais Ikulu ina jukumu la kusimamima Afisi ya Faragha ya Mheshimiwa Rais, Afisi ya Baraza la Mapinduzi,Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Idara ya Utumishi na Uendeshaji, Idara ya Mawasiliano na Habari, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Shughuli za Wazanzibari Wanaoishi Nje ya Nchi, Afisi ya Usalama wa Serikali (GSO),Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu na Afisi ya Rais Ikulu - Pemba.

MAJUKUMU YA AFISI YA RAIS IKULU

8. Mheshimiwa Spika, Kutokana na mabadiliko yaliyofanyika Serikalini, Afisi ya Rais Ikulu itatekeleza majukumu yafuatayo:
i. Kusimamia shughuli za Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
ii. Kuhakikisha kuwa jamii inapata habari juu ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo na Sera zinazotekelezwa na Mheshimiwa Rais

BAJETI IKULU
4 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
iii. Kusimamia majukumu ya kikatiba na kisheria ya Baraza la Mapinduzi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi.
iv. Kusaidia uchambuzi wa Nyaraka na Sheria zinazotarajiwa kuwasilishwa serikalini pamoja na kufuatilia utekelezaji wake.
v. Kuratibu na kusimamia shughuli za Wazanzibari wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora).
vi. Kuratibu na kuandaa shughuli za Mipango,Sera na Utafiti katika Afisi ya Rais Ikulu.
vii. Kusimamia Nyaraka na Kumbukumbu zote za Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) kwa zile Taasisi zake zilizopo Zanzibar.
viii. Kupanga na kusimamia utekelezaji wa shughuli za Afisi ya Usalama wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (GSO).
9. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo ya utangulizi sasa naomba uniruhusu niwasilishe kwa ufupi Utekelezaji wa Programu za Afisi ya Rais Ikulu kwa kipindi cha Julai 2021 – Machi 2022.
10. Mheshimiwa Spika, Afisi ya Rais Ikulu kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ilitekeleza Programu kuu tano na ndogo 14 chini ya Mafungu mawili ambayo ni A01 na A02. Utekelezaji wa Programu hizi, ulizingatia Mipango Mikuu ya Kitaifa ikiwemo Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2020 - 2025, ZADEP, Hotuba ya Rais wa Zanzibar

BAJETI IKULU
5 Rais na Mwenyekiti wa Bararaza la Mapinduzi aliyoitoa katika ufunguzi wa Baraza la Kumi la Wawakilishi pamoja na miongozo, maelekezo na maagizo aliyoyatoa. Kupitia Programu zake, Afisi iliandaa Mpango Kazi wa mwaka 2021/2022 na kuweka vipaumbele katika mambo yafuatayo:-
a) Kuimarisha utendaji na umakini katika matumizi ya rasilimali za Serikali
11. Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuhimiza umakini katika nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kupiga vita vitendo vya rushwa na uhujumu wa uchumi. Ni imani yetu kuwa, umma na wadau wa
maendeleo wameshuhudia utumishi unaofuata sheria na uadilifu katika kuhudumia jamii pamoja na kuimarika kwa nidhamu za watendaji wa Serikali. Aidha, pamoja na mabadiliko hayo,Serikali inaendelea kuwahimiza watendaji wa Wizara, Idara na Taasisi zake kuzingati sheria na uwadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ili
kupata matokeo ya utumishi wenye ufanisi.
b) Kudumisha Amani na Utulivu Nchini
12. Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kupitia ziara na mikutano yake na makundi mbali mbali ya kijamii,ameendelea kuhimiza umuhimu wa kudumisha

BAJETI IKULU
6 Amani na utulivu. Kwa kutolea mfano tarehe 25 Machi, 2022 wakati alipokuwa akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu katika Masjid Arafa Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” aliwasisitiza wananchi kuendelea kuhubiri amani.
c) Kuimarika kwa Ushiriki wa Zanzibar katika masuala ya Mtangamano wa Kikanda na Jumuiya za Kimataifa
13. Mheshimiwa Spika, Afisi kupitia Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi Nje ya Nchi, imehakikisha kuwa Zanzibar inanufaika na uhusiano wa Jumuiya za Kikanda na Kimataifa. Katika kufikia hatua hii, wataalamu wamewezeshwa kushiriki katika vikao vya mtangamano wa kikanda na kimataifa,pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa na faida zinazotokana na Jumuiya hizo.
Aidha, Serikali inaendelea kuzihamasisha balozi na jumuiya za kimataifa kufungua Afisi ndogo za uwakilishi Zanzibar ili ziweze kiungo muhimu cha kukuza uwekezaji na upatikanaji wa masoko ya bidhaa katika nchi zao na kuvutia uwekezaji Zanzibar.
d) Uratibu wa Wazanzibari Wanaoishi Nje ya Nchi.
14. Mheshimiwa Spika, Afisi ya Rais Ikulu imeweka mazingira wezeshi na kuendelea kuratibu na kuhamasisha ushiriki wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) ili waweze kuzitangaza

BAJETI IKULU
7 Fursa zinazopatikana nchini na kushiriki kikamilifu katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu. Afisi imehakikisha kuwa, kupitia sheria namba 4 ya 2020, inayosimamia utekelezaji wa Sera ya Diaspora kwa mujibu wa miongozo iliyopo imewezesha wanadiaspora wa Zanzibar kushiriki ipasavyo katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
e) Kusimamia na Kutunza Nyaraka na Kumbukumbu.
15. Mheshimiwa Spika, Afisi ya Rais Ikulu, kupitia Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu imeendelea kufanya ukaguzi wa kumbukumbu na nyaraka kwa Wizara na Taasisi za Serikali. Aidha, imeweza kutoa huduma za utafiti kwa Watafiti wa ndani na Watafiti nje ya nchi. Vile vile Afisi imetangaza na kutoa taaluma kuhusu kazi, majukumu na umuhimu wa nyaraka zinazohifadhiwa na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar kupitia Maonesho ya Biashara ya kuadhimisha Sherehe za Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA AFISI YA RAIS IKULU KWA KIPINDI CHA JULAI – MACHI 2021/2022
16. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Afisi ya Rais Ikulu kupitia Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu ilipangiwa kukusanya TZS. 15.0 Milioni.

Inaendelea kwenye link ya PDF chini