Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya Uteuzi wa Viongozi katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar(SUZA) na Wakala wa Serikali wa Uchapaji katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

1). Profesa Moh'd Makame Haji ameteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
2). Dkt.Ali Makame Ussi ameteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha-Taaluma,Utafiti na Ushauri Elekezi (SUZA).
3). Bibi Kidawa Hamid Saleh ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Serikali wa Uchapaji
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 17 Novemba,2021.